Ugonjwa wa kidole tumbo

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023 | Imebadilishwa Mar 2023

Je, ugonjwa wa kidole tumbo ni nini?

Kidole tumbo chako ni tyubu ndogo yenye umbo la kidole inayopatikana mwishoni mwa utumbo wako mpana. Ugonjwa wa kidole tumbo ni uvimbe unaosababisha kidole tumbo chako kuvimba na kupata maambukizi.

  • Ugonjwa wa kidole tumbo ni tatizo linalotokea sana

  • Dalili za kawaida ni maumivu ya tumbo, kuhisi kichefuchefu, na homa

  • Madaktari hutibu ugonjwa wa kidole tumbo kwa upasuaji na dawa za kuua bakteria

Ugonjwa wa kidole tumbo usipotibiwa, kidole tumbo chako kinaweza kupasuka. Hali hii husababisha maambukizi kwenye tumbo lako yaitwayo peritonitisi. Uvimbe wa ngozi ya fumbatio unaweza kutishia maisha.

(Angalia pia Ugonjwa wa Kidole Tumbo kwa Watoto.)

Je, ugonjwa wa kidole tumbo husababishwa na nini?

Ugonjwa wa kidole tumbo husababishwa wakati kitu, kama vile kipande kidogo cha kinyesi kigumu (haja kubwa) kimeziba kidole tumbo chako. Uzibaji huu husababisha maambukizi na kuvimba.

Je, dalili za ugonjwa wa kidole tumbo ni zipi?

Dalili za ugonjwa wa kidole tumbo ni pamoja na:

  • Maumivu yanayoanza katika sehemu ya katikati ya eneo la tumbo la juu na kuhamia kwenye sehemu ya chini kulia kwenye tumbo yako

  • Maumivu yanayozidi taratibu kwa kipindi cha siku moja au mbili

  • Maumivu huongezeka ukisogea au ukikohoa au mtu anapobonyeza sehemu yenye maumivu

  • Kupoteza hamu ya kula

  • Kuhisi mgonjwa tumboni na kutapika

  • Wakati mwingine homa ya nyuzi 100 hadi nyuzi 101 Farenhaiti (nyuzi 37.7 hadi nyuzi 38.3 Selsiasi)

Kwa watu wengi na kwa watoto wachanga na wakubwa:

  • Maumivu yanaweza kutokea kwenye tumbo yote, si tu upande wa chini kulia

Kwa watu wazee na kwa wanawake wajawazito:

  • Huenda maumivu yasiwe makali sana na eneo la tumbo lisiwe na maumivu sana linapoguswa

Kidole tumbo chako kikipasuka:

  • Huenda usiwe na maumivu makubwa kwa saa kadhaa

  • Kisha, maumivu yataongezeka

  • Maambukizi yanaweza kuenea ndani ya tumbo yako (hali inayoitwa uvimbe wa ngozi ya fumbatio)

  • Maambukizi yanaweza kuenea kwenye mtiririko wako wa damu na kusababisha baadhi ya ogani zako kuacha kufanya kazi kwa njia ya kawaida (sepsis) na shinikizo la damu yako kupungua hadi kiwango hatarishi (mshtuko wa sepsisi)

Madaktari wanawezaje kujua iwapo nina ugonjwa wa kidole tumbo?

Madaktari wakati mwingine hutambua ugonjwa wa kidole tumbo kulingana na dalili zako na uchunguzi wa mwili. Lakini pia kwa kawaida wanafanya:

Kuna uwezekano zaidi wakatumia kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa watoto na uchanganuzi wa CT kwa watu wazima.

Je, ugonjwa wa kidole tumbo hutibiwa vipi?

Madaktari hutibu ugonjwa wa kidole tumbo kwa kutumia:

  • Upasuaji wa kuondoa kidole tumbo chako kwa kukata wazi sehemu ya tumbo au kufanya laparoskopi

  • Kukupa dawa za kuua bakteria moja kwa moja kwenye mishipa (IV)

Ikiwa tayari kidole tumbo chako kimepasuka wakati wa upasuaji, utahitaji kukaa hospitalini ili upate majimaji na dawa za kuua bakteria kwa njia ya mshipa kwa muda mrefu zaidi ili kuzuia sepsisi.