Divertikulaitisi

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2024

Utumbo wako ni mrija mrefu katika mfumo wa usagaji chakula ambao humeng'enya chakula na kufyonza virutubishi. Una utumbo mpana na utumbo mdogo. Utumbo wako mpana (utumbo mkubwa) unaunganisha utumbo wako mdogo na rektamu yako (pochi katika sehemu ya mwisho ya utumbo wako mpana mahali kinyesi kinapohifadhiwa hadi pale utakapojisaidia). Vifuko au pochi ndogo (divatikula) zinaweza kuundwa kwenye utumbo wako mpana na hii inaitwa divertikula. Kuna uwezekano mkubwa kuwa husababishwa na shinikizo la juu kwenye utumbo.

Divertikulaitisi ni nini?

Divertikulaitisi ni tatizo la divertikula. Divertikulosisi ni kuvimba kwa divertikula.

  • Dalili zinajumuisha maumivu kwenye sehemu ya chini kushoto ya tumbo yako, wororo na homa

  • Madaktari hutambua divatikulaitisi kwa kutumia uchanganuzi wa CT

  • Matibabu yanajumuisha mapumziko, lishe ya kiowevu na dawa za kuua bakteria

  • Ikiwa una dalili kali, unaweza kuhitaji kusalia hospitalini na wakati mwingine upasuaji

Utumbo Mpana wenye Divatikula

Divatikula ni mifuko inayofanana na puto ambayo inaweza kukua kwenye utumbo mpana.

Nini husababisha divertikulaitisi?

Divatikulaitisi hutokea kwa watu ambao wana divatikulosisi, hali ambapo pochi na vifuko huundwa kwenye utumbo wako mpana.

Sababu halisi haijaeleweka kikamilifu. Wakati mwingine, kinyesi na bakteria huingia kwenye mojawapo ya vifuko (divertikula), hivyo kusababisha uvimbe na maambukizi.

  • Divatikulaitisi kwa kawaida ni sehemu ya chini zaidi ya utumbo wako mpana

  • Divertikulaitisi kwa sana huwa kali zaidi kwa watu wazee na watu wanaotumia kotikosteroidi

Ikiwa una divertikula, una hatari ya juu ya kupata divertikulaitisi ikiwa:

  • Zaidi kwa umri

  • Una uzani mkubwa kupita kiasi

  • Haufanyi mazoezi

  • Kuvuta sigara

  • Unakula lishe yenye mafuta mengi, yenye ufumwele kidogo

  • Unatumia dawa fulani, kama vile kotikosteroidi, dawa za maumivu za opioid na dawa kumaliza uvimbe

Dalili za divertikulaitisi ni zipi?

Divertikulaitisi husababisha:

  • Maumivu kwenye sehemu ya chini ya kushoto ya tumbo yako

  • Wororo

  • Homa

Divertikulaitisi inaweza kusababisha matatizo kama vile:

  • Usaha (mkusanyiko wa udusi)

  • Maambukizi kwenye viungo vilivyo karibu au kwenye nafasi ya tumbo kati ya viungo (peritonitis)

  • Maambukizi makali kwenye damu yako yanayosababisha viungo vingine kutofanya kazi vizuri (sepsis)

  • Kizuizi cha utumbo kutokana na kupata kishikizo kwenye utumbo

  • Fistula (muunganisho usio wa kawaida kati ya viungo viwili ambavyo havipaswi kuunganisha, kama vile utumbo na kibofu cha mkojo)

Baadhi ya Matatizo ya Divertikulaitisi

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina divertikulaitisi?

Kwa kawaida madaktari hufanya vipimo kama vile:

  • Uchanganuzi wa CT

  • Vipimo vya damu ili kuangalia maambukizi na sababu zingine za maumivu ya tumbo

Je, madaktari hutibu divertikulaitisi vipi?

Unaweza kutibu divertikulaitisi isiyo kali nyumbani kwa kutumia:

  • Kupumzika

  • Lishe maalum—kula viowevu pekee kwa siku chache, kama vile mchuzi wa nyama, juisi au maji na kisha kuongeza polepole vyakula vyepesi kama vile mayai, mboga zilizopikwa au mtindi

  • Dawa ya maumivu

  • Wakati mwingine, dawa za kuua bakteria

Ikiwa una dalili kali zaidi, unaweza kuhitaji kusalia hospitalini kwa ajili ya matibabu. Matibabu yako yanaweza kujumuisha:

  • Viowevu na dawa za kuua bakteria kwenye mshipa wako

  • Dawa ya maumivu

  • Kupumzika kitandani

  • Kutokula chakula hadi dalili zako ziache

  • Wakati mwingine, kuweka sindano kupitia ngozi ili kuondoa maambukizi yaliyo kwenye kifuko cha usaha (jipu)

Unaweza kuhitaji upasuaji wa dharura ikiwa:

  • Dalili zako haziimariki au kuwa mbaya zaidi

  • Una maumivu yanayoongezeka, wororo na homa

  • Utumbo wako umezuiwa

  • Utumbo wako unapasuka, hivyo husababisha maambukizi kwenye utando wa tumbo yako (peritonitis)

  • Una usaha ambao unahitaji kutolewa

Daktari wako huondoa sehemu iliyoraruka (kupasuka) ya utumbo wako. Kisha daktari wako aidha ataunganisha upya utumbo wako au kukupea kolostomia ya muda. Kolostomia ni mpenye wa upasuaji kwenye tumbo yako uliounganishwa kwa mojawapo ya utumbo wako. Kinyesi hutoka kwenye mfuko wa kolostomia wakati utumbo wako unapona.

Fistula ambayo inaundwa inaweza pia kutibiwa kwa upasuaji.

Mwezi mmoja hadi 3 baada ya wewe kujihisi vizuri, kwa kawaida madaktari hufanya kolonoskopia (kipimo ambapo daktari huingiza mpira mwembamba, mwepesi ulio na kamera ndogo zaidi kupitia kwenye rektamu ili kuangalia utumbo wako mpana) ili kuondoa uwezekano wa kuwa na saratani ya utumbo mpana kama kisababishaji cha msingi cha dalili zako za awali.

Daktari pia atakuekeleza:

  • Kula chakula chenye fumwale zaidi

  • Mazoezi

  • Kupunguza uzani ikiwa una uzani mkubwa kupita kiasi

  • Kutovuta sigara

Ni muhimu kupigia daktari wako simu ikiwa dalili za divertikulaitisi zinatokea tena.