Divertikulosis

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2024

Utumbo wako ni mrija mrefu katika mfumo wa usagaji chakula ambao humeng'enya chakula na kufyonza virutubishi. Una utumbo mdogo na utumbo mpana. Utumbo wako mpana (utumbo mkubwa) unaunganisha utumbo wako mdogo kwenye rektamu yako (pochi katika sehemu ya mwisho ya utumbo wako mpana mahali kinyesi kinapohifadhiwa hadi pale utakapojisaidia).

Divertikula ni nini?

Katika divatikulosisi, kifuko au pochi ndogo zaidi hujiunda kwenye utumbo wako mkubwa. Mifuko hii inaitwa divertikula.

  • Divertikula inatokea kwa sana vile watu wanazeeka na kufikia umri wa miaka 90 watu wengi wana divertikula

  • Kwa kawaida divertikula haisababishi dalili isipokuwa divertikula moja ikivuja damu

  • Divertikulaitisi ni hali inayosikika kufanana ambapo mojawapo ya divertikula yako inavimba na kuwa na maumivu

  • Madaktari hutambua divertikula wakati wanafanya kolonoskopia au eksirei ili kuangalia matatizo mengine

  • Kula lishe yenye ufumwele kunaweza kuzuia mifuko zaidi isitengenezwe

Utumbo Mpana wenye Divatikula

Divatikula ni mifuko inayofanana na puto ambayo inaweza kukua kwenye utumbo mpana.

Ni nini husababisha divertikula?

Divatikulosisi ina uwezekano mkubwa wa kusababishwa na shinikizo la juu kwenye utumbo wako. Lishe yenye ufumwele kidogo inaweza kusababisha shinikizo lililoongezeka. Shinikizo lililoongezeka hufanya sehemu dhaifu kwenye ukuta wa utumbo wako kuvimba, kuunda mfuko au pochi.

Divertikula kwa kawaida hufanyika baada ya umri wa miaka 40. Huwa inatokea kwa sana vile unazeeka. Karibu watu wote ambao wanafika umri wa miaka 90 wana divertikula.

Je, dalili za divertikula ni zipi?

Watu wengi walio na divertikula hawana dalili isipokuwa wakati mwingine wanaweza kuhisi:

  • Kufunga choo

  • Maumivu ya tumbo ya mkakamao

  • Kuvimbiwa

Vinginevyo, una uwezekano mkubwa wa kukosa kuonyesha dalili isipokuwa ukipata matatizo kama vile divertikulaitisi au kuvuja damu.

Wakati mwingine, mojawapo ya kifuko huvuja damu, kusababisha damu kuwa kwenye kinyesi chako. Kwa kawaida kuvuja damu huacha kwenyewe, lakini inaweza kuwa kwa kiwango kikubwa.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina divertikula?

Madaktari hupata ugonjwa wa divertikulosisi wanapofanya vipimo kwa sababu zingine, kama vile maumivu ya tumbo, kuvuja damu, au uchunguzi wa saratani ya utumbo mpana. Divertikula inaweza kuonekana kwenye vipimo vifuatavyo:

Je, madaktari hutibu vipi divertikula?

Madaktari hawatibu divertikula yenyewe, lakini wanaweza kujaribu kuzuia matatizo yake kwa kupunguza shinikizo kwenye utumbo wako. Watakwambia:

  • Ule lishe yenye ufumwele mwingi (mboga, matunda na nafaka nzima nyingi)

  • Kunywa vinywaji kwa wingi

  • Wakati mwingine, ule kapi au utumie virutubishi ili kufanya kinyesi kiwe kigumu kiasi

Kuvuja damu kwingi huacha bila matibabu. Kusipoacha, madaktari mara nyingi hufanya kolonoskopia ili:

  • Kufunga sehemu inayovuja damu kwa kutumia joto au leza

  • Kuchoma sindano yenye dawa kwenye sehemu hio

Ikiwa matibabu ya kolonoskopia hayasitishi kuvuja damu, madaktari wanaweza kufanya angiografia. Katika angiografia, wanaingiza mfereji mdogo kupitia mojawapo ya mishipa yako ya damu hadi kwenye sehemu inayovuja damu. Kisha wanakuchoma sindano ya kitu kinachozuia mshipa wa damu unaovuja damu. Watu kwa nadra huhitaji upasuaji ili kusitisha kuvuja damu.