Mambukizi ya Helikobakta pilori ni nini?
Maambukizi ya Helikobakta pilori ni maambukizi ya bakteria ambayo inasababisha kuvimba kwa utando wa tumbo yako na vidonda (vidonda) kwenye tumbo au utumbo wako. Mara nyingi hufupishwa iwe H. pylori.
Maambukizi ya H. pylori yanaweza kusababisha uvimbe tumboni na ugonjwa wa vidonda vya pepsini. Ikiwa maambukizi ya H. pylori hayatatibiwa, inaongeza uwezekano wako kupata saratani ya tumbo.
Maambukizi haya yanasababishwa na aina ya bakteria inayoitwa Helikobakta pilori
Ni maambukizi ya kawaida sana—kufikia umri wa 60, takriban nusu ya watu wameambukizwa
H. pylori huenea kutoka kwa mtu hadi mwingine kupitia kupiga busu, mgusano wa karibu na kutoosha mikono baada ya kutoa kinyesi (kinyesi)
Watu wengi hawana dalili, lakini wanaweza kuwa na maumivu kwenye eneo la tumbo ya juu
Madaktari hutibu maambukizi ya H. pylori kwa kutumia dawa za kuua bakteria
Dalili za maambukizi ya H. pylori ni zipi?
Huenda usiwe na dalili zozote. Ikiwa una dalili, zinajumuisha:
Maumivu katika tumbo yako ya juu
Kushindwa kumeng'enya chakula
Kuhisi vibaya tumboni (kuhisi gesi, kuhisi kujaa au mwasho)
Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nina maambukizi ya H. pylori?
Madaktari hushuku maambukizi ya H. pylori kutokana na dalili zako. Ili kujua kwa hakika, watafanya vipimo kama vile:
Vipimo vya mpumuo au kinyesi
Endoskopia ya juu (kwa kutumia mfereji wa kutazama unaopinda ili kuangalia kwenye tumbo yako)
Madaktari hutibu maambukizi ya H. pylori vipi?
Madaktari hutibu maambukizi ya H. pylori kwa kutumia:
Dawa za kuua bakteria
Dawa ili kupunguza asidi kwenye tumbo (kizuizi cha pampu ya protoni)
Baada ya matibabu, madaktari watarudia vipimo vya mpumuo au kinyesi ili kuhakikisha kuwa maambukizi yameisha.