Dalili za Tahadhari za Saratani

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Baadhi ya dalili zinaweza kuwa ishara za tahadhari za saratani Mara nyingi, watu walio na dalili hizi hawana saratani. Lakini kwa kuwa inawezekana zaidi kutibu kansa madaktari wanapoitambua mapema, ni muhimu kumwambia daktari wako iwapo una dalili zozote za tahadhari.

Ni zipi ishara za tahadhari za saratani?

Nenda kwa daktari iwapo una dalili hizi za tahadhari za saratani—matibabu hufanya kazi vizuri zaidi yakianzishwa mapema:

  • Kupungua uzani bila sababu inayofahamika

  • Uchovu na kuchoka

  • Kutokwa jasho usiku

  • Kupoteza hamu ya kula au kutohisi njaa

  • Maumivu mapya ambayo hayakwishi

  • Kuhisi kichefuchefu tumboni (au kutapika) kunakorudi mara kwa mara

  • Damu kwenye mkojo au kinyesi (haja kubwa)

  • Mabadiliko kwenye kinyesi chako (kuwa kigumu mno au majimaji mno)

  • Homa inayorudi mara kwa mara

  • Kikohozi kisichoisha

  • Mabadiliko kwenye ukubwa au rangi ya kiwaa cheusi

  • Doa kwenye ngozi yako ambalo haliponi

  • Tezi limfu ambazo ni kubwa kuliko kawaida (uvimbe mgumu chini ya mikono yako au kwenye shingo)

  • Uvimbe kwenye matiti