Viwaa vyeusi ni nini?
Viwaa vyeusi ni uvimbe mdogo kwenye ngozi ambao unaweza kuwa popote mwilini mwako. Kwa kawaida huwa vya rangi nyeusi na vya mviringo au umbo la yai. Karibu kila mtu ana viwaa vyeusi kadhaa.
Mara nyingi viwaa vyeusi hutokea kwanza wakati uko mtoto au kijana
Huwa haviishi vyenyewe
Viwaa vyeusi havina maumivu au mwasho
Kwa kawaida hazihitaji matibabu, isipokuwa kama zinakusumbua
Viwaa vyeusi si saratani. Hata hivyo, aina ya saratani ya ngozi inayoitwa melanoma wakati mwingine huanzia kwa kiwaa cheusi. Ishara za onyo la saratani zinajumuisha kiwaa cheusi:
Inazidi kuwa kubwa
Kubadilisha umbo
Kubadilisha rangi
Ona daktari ikiwa una kiwaa cheusi ambacho kimebadilika.
Viwaa vyeusi vinakaa aje?
Kwa kawaida viwaa vyeusi:
Vinatofautiana kwa ukubwa, kuanzia alama ndogo hadi zaidi ya inchi moja (takriban sentimita 2 1/2) kwa ukubwa
Vinalingana, kumaanisha kuwa ukaweza chora mstari kupita katikati, nusu hizo mbili zitalingana
Ni vya mviringo au umbo la yai
Vinaweza kuwa sawasawa au zimeinuka, nyororo au ngumu au nywele zinamea kutoka kwake
Vinaweza kuwa vyekundu kwanza lakini mara nyingi hugeukia kuwa vya rangi ya tan, manjano, kahawia, buluu-kijivu au kukaribia rangi nyeusi
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Viwaa vyeusi ambavyo si vya kawaida ("viwaa vyeusi vya aina yake"):
Vina mazoea ya kuwa vya zaidi ya rangi moja, haswa kahawia na tan na mandharinyuma ya waridi
Vina umbo na kingo zisizolingana
Mara nyingi huwa kubwa zaidi kuliko viwaa vyeusi kwenye mwili wako
Kwa kawaida hutokea kwenye ngozi ambayo hupata jua lakini vinaweza kuwa mahali popote mwilini mwako
Viwaa vyeusi vya aina yake vina mazoea ya kuendelea kwenye familia. Watu walio na hata viwaa vyeusi vichache vya aina yake wana uwezekano wa juu zaidi wa kupata melanoma.
Ni lini napaswa kuona daktari kuhusu kiwaa cheusi?
Nenda kwa daktari aangalie kiwaa cheusi:
Kikiwa na maumivu au mwasho
Kikivuja damu
Kikibadilisha umbo, kikikua au kikiwa pana zaidi kuliko kifutio cha penseli
Kikibadilisha rangi, kikiwa na rangi zisio za kawaida au ni cheusi zaidi au kina rangi tofauti na viwaa vyeusi vingine vyako
Ikiwa hakina umbo sawa pande zote mbili
Ikiwa kina mipaka ambayo si ya mviringo au umbo la yai
Ikiwa kinatokea wakati uko na umri wa miaka 30 au zaidi
Madaktari hutibu vipi viwaa vyeusi?
Viwaa vyeusi vingi havina madhara na havihitaji matibabu. Daktari wako anaweza kuondoa viwaa vyeusi ambavyo vinakusumbua.
Daktari wako atafanya:
Angalia kwa karibu viwaa vyeusi vyako
Angalia ikiwa kiwaa cheusi cha aina yake ni chenye saratani kwa kukagua sehemu yake chini ya hadubini (uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi)
Fanyiwa upasuaji ili kuondoa kiwaa cheusi (ikiwa ni chenye saratani) na ngozi iliyo kando ya kiwaa cheusi
Ninawezaje kuzuia melanoma?
Melanoma ni saratani sugu ya ngozi, yenye kutishia maisha. Angalia viwaa vyeusi kwa mabadiliko yoyote. Nenda kwa daktari aangalie viwaa vyeusi ambavyo vimebadilika:
Uko kwa hatari ya juu zaidi ya kupata melanoma ikiwa:
Una viwaa vyeusi vya aina yake
Una aidi ya viwaa vyeusi 50
Una mwanafamilia ambaye amewahi kuwa na melanoma
Ikiwa uko katika hatari ya juu zaidi ya kupata melanoma, madaktari wanaweza kutaka:
Ngozi yako iangaliwe angalau mara moja kwa mwaka na dermatologist (daktari wa ngozi)
Viwaa vyeusi vyako vyovyote vya aina yake ambavyo vimebadilika viondolewe mara moja
Kwa sababu uharibifu wa ngozi uliosababishwa na jua huongeza hatari yako ya kupata melanoma (na pia saratani zingine za ngozi), hakikisha:
Umeepuka kubabuka kwa jua na kuchomwa na jua
Umeepuka kuwa nje kwenye jua kati ya saa 10:00 asubuhi na 3:00 jioni
Umejipaka mafuta ya kukinga miale ya jua kwenye ngozi iliyo wazi kwa jua
Umevalia kofia na mavazi ambayo hukulinda kutokana na jua