Dematofibromasi ni nini?
Dematofibromasi ni uvimbe mdogo wenye rangi nyekundu-kahawia kwenye ngozi yako. Kwa kawaida huwa vidogo kuliko upana wa nusu inchi (takriban sentimita 1)
Dematofibromasi hazina madhara
Ni za kawaida kwa watu wazima, haswa wanawake
Dematofibromasi zinasababishwa na jeni fulani unayorithi kutoka kwa wazazi wako. Baadhi ya watu wanapata nyingi.
Dermatofibroma
MAKTABA YA PICHA ZA KISAYANSI
Dalili za dematofibromasi ni zipi?
Uvimbe mdogo thabiti, mara nyingi kwenye mapaja au miguu yako
Kwa kawaida hakuna dalili, lakini kwa matukio ya nadra zinamwasho
Madaktari hutibu dematofibromasi vipi?
Kwa kawaida, madaktari hawautibu.
Dermatofibromasi ikikuwa kubwa zaidi au ikikusumbua, daktari wako anaweza kuukata kwa kutumia skapo (kisu cha upasuaji).