Nyenzo za Mada
Keloidi ni nini?
Keloidi ni tishu ya alama iliyokuwa kuzidi. Zinakaa ngozi iliyoinuka inayong'aa.
Keloidi zinaundwa miezi baada ya jeraha
Huwapata zaidi watu wenye ngozi nyeusi
Ni nini husababisha keloidi?
Aina yoyote ya jeraha la ngozi linaweza kusababisha keloidi, kama vile:
Mivunjiko ya ngozi
Upasuaji
Chunusi
Wakati mwingine, keloidi hujiunda kwa sababu isiyo wazi.
Keloidi zinakaa aje?
Keloidi ni:
Ziko juu ya ngozi yako, kama robo inchi (takriban nusu sentimita) juu zaidi
Zinang'aa, ni ngumu na laini
Ngozi nyeusi au zenye rangi kiasi ya waridi
Keloidi zinaweza kuwasha au kuweza kuhisi lakini haziumi.
Madaktari hutibu keloidi vipi?
Matibabu ya kuondoa keloidi hayafanyi kazi vizuri. Madaktari wanaweza kujaribu kufanya keloidi ziwe laini kwa kuzichoma sindano iliyo na dawa inayoitwa kotikosteroidi.
Madaktari wanaweza pia kutumia upasuaji au leza ili kuondoa keloidi. Hata hivyo, kwa sababu keloidi huanza kwa alama, mara nyingi keloidi hukua tena. Wakati mwingine hukua tena hata kubwa zaidi. Baadhi ya dawa mpya ambazo zinapunguza kasi ya mfumo wako wa kingamwili zinaweza kusaidia kukomesha keloidi kurudi tena. Kuvalia viraka maalum au mavazi yanayobana (mavazi yanayobana, maalum) ambayo yanabana kwenye keloidi pia kunaweza kusaidia kuzikomesha zisirudi.