Hemangioma ni nini?
Hemangioma ni ukuaji wekundu kwenye ngozi yako. Ni bonge la mishipa ya damu midogo sana.
Hemangioma ni za kawaida kwa watoto na mara nyingi zinaitwa alama za kuzaliwa za matunda ya storoberi
Hemangioma zinaweza kukua mahala popote, lakini mara nyingi kwenye kichwa au shingo ya mtoto
Zinakua hadi mtoto wako anakuwa wa takriban mwaka mmoja
Kisha, zinaanza kupungua kwa ukubwa na kwa kawaida zinaisha kwa wakati ambao mtoto wako ako na 10
Wakati hemangioma inaisha, ngozi ya mahali ambapo zilikuwa mara nyingi huwa pa rangi tofauti au kuacha alama
Watu wazima wanaweza kupata Hemangioma (hizi mara nyingi zinaitwa uvimbe la cherry). Ni za kawaida na hazina madhara.
© Springer Science+Business Media
Hemangioma husababishwa na nini?
Hakuna anayejua ni nini husababisha bonge la mishipa ya damu kuunda hemangioma.
Dalili za hemangioma ni zipi?
Kuna sehemu yenye uvimbe ya buluu au wekundu angavu
Hazina mwasho au si chungu
Jeraha ndogo linaweza kufanya hemangioma kuvuja damu na kuunda kidonda
Kidonda kinaweza kuuma na kuchukua muda kupona
Hemangioma inayokua karibu na jicho inaweza kuzuia uwezo wa kuona
Hata kama hemangioma hazisababishi matatizo yoyote ya kimatibabu, huenda usipende zinavyokaa.
Je, madaktari hutibu vipi hemangioma?
Hemangioma nyingi hupungua kwa ukubwa na huisha zenyewe. Hemangioma kwa kawaida huanza kupungua kwa ukubwa wakati mtoto ana umri wa miaka 12 hadi 18. Kwa takriban watoto 7 kati ya 10, hemangioma huisha wakifika umri wa miaka 7.
Kwa sababu kwa kawaida hemangioma huisha zenyewe, madaktari hawazitibu isipokuwa zikisababisha matatizo. Ikiwa hemangioma inaifanya ngumu kuona au kupumua au inasababisha matatizo mengine, madaktari:
Watatoa dawa (kama vile propranolol au kotikosteroidi) ili kusaidia kupunguza ukubwa wa hemangioma
Wakati mwingine, watafanya matibabu ya leza kwenye hemangioma
Kidonda kisipopona haraka zaidi, daktari wanakitibu kwa kutumia vazi na krimu maalum.
Kwa kawaida madaktari huwa hawafanyi upasuaji ili kuondoa hemangioma kwa sababu hio inaweza kuacha alama. Alama inaweza kusumbua sana kama hemangioma.
Uvimbe la cherry, unaopatikana kwa watu wazima, hauhitaji matibabu. Zikikusumbua, daktari anaweza kuziondoa kwa sindano ya umeme au skapo (kisu kidogo cha kupasulia).