Madoa ya Mvinyo

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Madoa ya mvinyo ni nini?

Madoa ya mvinyo ni alama za waridi, nyekundu au za zambarau kwenye ngozi. Alama nyingi kama hizo zina rangi inayofanana na divai nyekundu nzito tamu. Alama hizo zimetengenezwa na mishipi ya damu mingi midogo ambayo imekua isivyofaa.

  • Madoa ya mvinyo ni aina ya alama za kuzaliwa, kwa hivyo watoto wanazaliwa nazo

  • Madoa ya mvinyo hayajiondoi yenyewe

  • Madoa ya mvinyo katika sehemu ya nyuma ya shingo ya mtoto aliyezaliwa karibuni wakati mwingine yanapewa jina la utani "alama za kung'atwa na korongo "

  • Hazina uchungu au mwasho, lakini baadhi ya watu wanasumbuliwa na jinsi zinavyokaa

Kwa nadra, madoa ya mvinyo kwenye uso wa mtoto ni ishara ya tatizo ambalo linaweza kusababisha kifafa na matatizo mengine ya afya. Tatizo hili linaitwa ugonjwa wa Sturge-Weber.

Dalili za madoa ya mvinyo ni zipi?

Madoa ya mvinyo:

  • Yako kwa ulalo, hayajainuka/wima

  • Ni ya rangi ya zambarau, nyekundu au waridi na yanweza kuwa nyeusi vile mtoto anakua

  • Yako kwenye sehemu ndogo au kubwa ya ngozi

Madaktari hutibu vipi madoa ya mvinyo?

Madoa ya mvinyo hayana madhara. Baadhi yao yanaweza kufunikwa kwa kutumia vipodozi ikiwa haupendezwi na jinsi yanakaa.

Madaktari wanaweza kufanya madoa ya mvinyo yapauke au kuisha kwa kutumia tiba ya leza. Kwa tiba ya leza, mwali mkali wa mwanga unalengwa kwenye doa la mvinyo. Matibabu haya hufanya kazi vizuri zaidi kwa watu wachanga zaidi.