Vishikizo vya ngozi ni nini?
Vishikizo vya ngozi ni nyororo, vishikizo vidogo kwenye ngozi yako. Kwa kawaida huwa ni za rangi sawa kama ngozi yako au nyeusi kidogo.
Vishikizo vya ngozi kwa kawaida huwa kwenye:
Shingo yako
Makwapa yako
Sehemu ya kinena chako (sehemu katikati ya tumbo na miguu yako ya juu)
© Springer Science+Business Media
Je, vishikizo vya ngozi husababisha matatizo?
Wakati mwingi, vishikizo vya ngozi havisababishi matatizo. Lakini huenda usipendezwe na jinsi vinakaa. Wakati mwingine mavazi au ngozi inaweza kugusana dhidi ya vishikizo vya ngozi, hivyo kuvifanya vivunje damu au kuuma.
Madaktari hutibu vipi vishikizo vya ngozi?
Kwa kawaida, vishikizo vya ngozi havihitaji matibabu. Ukitaka kishikizo cha ngozi kitolewe, madaktari wanaweza kufanya hivyo kwa urahisi kwa:
Kukigandisha kwa kutumia kiowevu cha naitrojeni
Kukikata
Kukichoma kwa kutumia sindano ya umeme