Limfanjioma ni nini?
Limfanjioma ni uvimbe kwenye ngozi uliojawa wa kiowevu safi au chenye damu. Zinasababishwa na mishipa ya limfu iliyokua kupita kiasi. Mishipa ya limfu husafirisha limfu mwili mzima. Limfu ni kiowevu safi kinachojumuisha seli nyeupe za damu ambazo husaidi mwili kupigana na maambukizi.
Limfanjioma si za kawaida
Kwa kawaida hutokea kati ya kipindi cha kuzaliwa na umri wa miaka 2
Si zenye saratani
DKT P. MARAZZI/MAKTABA YA PICHA ZA KISAYANSI
Dalili za limfanjioma ni zipi?
Zinaweza kutokea kama uvimbe mdogo au kama uvimbe mkubwa ambao huharibu umbo la mwili
Kwa kawaida huwa za rangi inayofanana na manjano, lakini chache ni za uwekundu au zambarau
Hazina mwasho au uchungu
Hutoa kiowevu safi au chenye rangi ya waridi kikitombolewa
Madaktari hutibu vipi limfanjioma?
Kwa kawaida limfanjioma hazihitaji matibabu.
Upasuaji ili kuondoa limfanjioma haupendekezwi. Limfanjioma zinakua ndani sana na kwa upana chini ya ngozi na mara nyingi huwa zinakua tena baada ya upasuaji.