Payojeniki granuloma ni nini?
Payojeniki granuloma ni uvimbe ulioinuliwa wa mviringo kwenye ngozi.
Una rangi ya wekundu wa damu au wekundu-kahawia
Payojeniki granuloma zinaweza kuwa mbichi, nyevunyevu au zenye ngozi ngumu
Hazina madhara lakini mara nyingi huvuja damu unapozifinya au kuzikuna
Zinaweza kuisha zenyewe au daktari anaweza kuhitaji kuziondoa
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Payojeniki granuloma husababishwa na nini?
Payojeniki granuloma huunda wakati mishipa midogo ya damu inayoitwa kapilari inakua kwa ukubwa zaidi kuliko kawaida na tishu iliyo kando yake inavimba.
Payojeniki granuloma zinauwezekano mkubwa wa kutokea:
Baada ya jeraha kwenye ngozi yako
Ukiwa mjamzito
Wakati wa ujauzito, wakati mwingine zinajiunda kwenye ufizi wako. Hili likifanyika zinapewa jina la utani "uvimbe wa ujauzito."
Dalili za payojeniki granuloma ni zipi?
Payojeniki granuloma:
Hukua haraka zaidi
Zimeinuka juu ya ngozi
Haziumi
Huvuja damu kwa urahisi zikigongwa au kukunwa
Madaktari hutibu vipi payojeniki granuloma?
Wakati mwingine payojeniki granuloma huisha bila matibabu
Zisipoisha, daktari wako anaweza kuzitoa kwa kufanya upasuaji au kwa kutumia sindano ya umeme
Zinaweza kukua tena baada ya kutolewa.