Keratosi ya seborrheic

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024
Nyenzo za Mada

Keratosi ya seborrheic ni nini?

Keratosi ya seborrheic ni vishikizo vya rangi ya tan, mchanga, kahawia au nyeusi kwenye ngozi ambavyo vinaweza kuonekana kama chunjua kubwa.

  • Keratosi ya seborrheic ni vishikizo visivyo na madhara ambavyo ni vya kawaida kwa watu wa umri wa kati na wazee

  • Si zenye saratani na hazitakuwa saratani

  • Wakati mwingine zinamwasho kidogo, lakini haziumi

  • Zikikusumbua, daktari anaweza kuziondoa kwa kuzidandisha au kutumia sindano ya umeme

Baadhi ya watu wanapata vishikizo vingi.

Ni nini husababisha keratosi ya seborrheic?

Madaktari hawajui kinachosababisha keratosi ya seborrheic, lakini zinaendelezwa kwenye familia.

keratosi ya seborrheic zinakaa aje?

Keratosi ya seborrheic:

  • Ni za mviringo au umbo la yai

  • Zina rangi ya tan, mchanga, kahawia au nyeusi

  • Zinaonekana ni kama zimekwama kwenye ngozi

  • Kwa kawaida huhisiwa kama nta, magamba au kama chunjua

  • Hutokea popote kwenye mwili, lakini mara nyingi zaidi kwenye panja, kifua, mgongo na tumbo

Watu wenye ngozi nyeusi wakati mwingine hupata kiasi kikubwa cha uotaji kwenye mashavu yao, kwenye mfupa wa shavu.

Keratosi ya seborrheic zenye rangi nyeusi kahawia zinaweza kudhaniwa kuwa viwaa vyeusi au saratani ya ngozi inayoitwa melanoma.

Madaktari hutibu aje keratosi ya seborrheic?

Keratosi ya seborrheic hazihitaji matibabu.

Zikianza kuudhi, kuwa na mwasho au kama hupendezwi na jinsi zinakaa, madaktari wanaweza kuziondoa:

  • Kwa kuzigandisha kwa kutumia kiowevu cha naitrojeni

  • Kwa kutumia sindano ya umeme