Melanoma ni nini?
Melanoma ni aina ya saratani ya ngozi. Inaanzia kwenye seli za ngozi zinazoitwa melanositi. Melanositi inatengeneza dutu ya kahawia inayoipa ngozi rangi yake. Melanoma kwa kawaida huwa ni rangi nyeusi. Saratani inaweza kuanzia kwenye ngozi ya kawaida au kwenye kiwaa cheusi.
Melanoma kwa kawaida huwa inaanza kama kivimbe kipya kidogo chenye rangi nyeusi kwenye sehemu ya ngozi yako iliyokaa juani
Melanoma pia inaweza kuanza kwenye sehemu ya mwili wako ambayo haipati mwanga wa jua, kama vile ndani ya kinywa chako
Saratani inasambaa kwa urahisi kwenye sehemu zingine za mwili ambapo inaharibu tishu na kwa kawaida huwa ni ya kufisha
Kugundua melanoma, madaktari wataondoa kipande cha tishu kwa ajili ya uchunguzi, ambacho watakichunguza kwa kutumia hadubini
Ikiwa melanoma yako itagunduliwa mapema zaidi, upasuaji kwa kawaida unaweza kuitibu
Picha kwa hisani ya Gregory L. Wells, MD.
Melanoma haipatikani sana kama ilivyo saratani nyingine za ngozi. Hata hivyo, ni ya hatari sana.
Je, nani yuko katika hatari ya kupata melanoma?
Sababu zifuatazo za vihatarishi vinakufanya uwe na uwezekano zaidi wa kupata melanoma:
Kukaa kwenye jua kwa kipindi kirefu na kubabuka kwa jua
Kutumia vitanda vya kugeuza ngozi
Wanafamilia wenye melanoma au viwaa vingi vyeusi vyenye maumbo tofauti
Ngozi laini na yenye madoa kutokana na jua
Idadi kubwa ya viwaa vyeusi vyenye maumbo na rangi tofuati
Mfumo wa kingamaradhi ulio dhaifu
Je, dalili za melanoma ni zipi?
Melanoma inaweza kutofautiana kwa namna zinavyoonekana. Zinaweza kuwa:
Mabaka ya kahawia yenye mpaka uliochanika na vidoa vyeusis vidogo
Mabaka ya kahawia yaliyoinuka pamoja na madoa mekundu, meupe, meusi au ya bluu
Uvimbe mgumu mwekundu, mweusi au kijivu
Melanoma haupatikani sana kwa watu wenye ngozi nyeusi. Ikiwa mtu mwenye ngozi nyeusi ayapata melanoma, kwa kawaida huwa ni chini ya kucha za kwenye vidole vya mkono au mguu au kwenye viganja au makanyagio ya miguu.
Dalili za melanoma ni uvimbe wowote kwenye ngozi ambao:
Inazidi kuwa kubwa
Unakuwa mweusi
Umetuna (mwekundu na umevimba)
Wenye madoa na unabadilisha rangi
Kuvuja damu, au ngozi juu yake inapasuka
Inawasha, laini au ina maumivu
Madaktari wanawezaji kujua ikiwa nina melanoma?
Madaktari watafanya biopsi (wataondoa sampuli ya tishu yako ili kuichunguza kwa kutumia hadubini).
IMRKU za melanoma
Ishara za onyo za melanoma wakati mwingine zinaitwa ABCDE za melanoma. Herufi IMRKU zinamaanisha:
Isopacha: nusu mbili za uvimbe wa ngozi hazina umbo linalofanana
Mipaka: uvimbe wa ngozi una mpaka uliochanika au unaingia kwenye ngozi ya eneo husika
Rangi: uvimbe wa ngozi unabadilisha rangi, hasa kuwa kahawia, nyeusi, nyekundu, nyeupe, bluu au rangi tofauti au nyeusi zaidi kuliko viwaa vyeusi vingine
Kipenyo: uvimbe wa ngozi ni mpana zaidi ya robo inchi (sentimita 0.64), mkubwa kuliko saizi ya kifutio cha penseli.
Ugeukaji: uvimbe wa ngozi unaonekana unapokuwa na umri wa zaidi ya miaka 30 au imekua au kubadilika hivi karibuni
Je, madaktari hutibu vipi melanoma?
Madaktari wanatibu melanoma kwa njia ya upasuaji kwa kukata na kuondoa uvimbe wa ngozi na angalau nusu inchi ya ngozi kwenye eneo la saratani. Ikiwa upasuaji hauwezekani, daktari wako atakupa dawa, kujaribu kuondoa uvimbe kwa baridi kali (matibabu kwa baridi) au akakupatia mionzi.
Ikiwa melanoma itasambaa kwenye maeneo mengine ya mwili wako, daktari wako anaweza kujaribu:
Upasuaji ili kuondoa tishu zenye saratani
Dawa ambazo husaidia mfumo wako wa kingamaradhi kuu saratani
Dawa ambazo zinatafuta na kuua seli za saratani ya melanoma
Ninawezaje kuzuia melanoma?
Unaweza kusaidia kuzuia melanoma kwa kupunguza muda wa kukaa kwenye nyua:
Jiepushe na jua—kaa kivulini, jaribu kuepuka jua kati ya saa 4:00 asubuhi na saa 10:00 jioni
Usiote jua wala kuingia kwenye mashine ya kufanya ngozi nyeusi
Vaa mavazi ya kujikinga, kama vile mashati ya mikono mirefu, suruali na kofia pana
Tumia mafuta ya kujikinga na jua ambayo yana angalau vipengele 30 vya ulinzi dhidi ya jua (SPF)—ni muhimu kutumia mafuta zaidi ya kuzuia jua kila baada ya saa 2 na baada ya kuogelea au kutokwa jasho
Nenda kwa daktari wako angalau mara moja kwa mwaka kwa ajili ya kuchunguza ngozi ikiwa:
Umewahi kuwa na melanoma hapo awali
Una viwaa vyeusi vingi
Mwone daktari ukiona mabadiliko ya upele kwenye ngozi baada ya wiki chache.