Nini kinachosababisha kasinoma ya seli za msingi?
Kasinoma ya seli za msingi ni aina iliyoenea sana ya saratani ya ngozi.
Watu wenye ngozi nyeupe wana uwezekano mkubwa wa kuipata kuliko wenye ngozi nyeusi
Kwa kawaida inakua kwenye ngozi ambayo imekaa juani
Madaktari kwa kawaida wanaondoa aina hii ya saratani ya ngozi kwa njia ya upasuaji, lakini wakati mwingine wanaitibu kwa kutumia tibakemikali au mionzi
Tofauti na saratani zingine, kasinoma ya seli za msingi ni vigumu sana kuenea kwenye maeneo mengine ya mwili au kukuua
Nini kinachosababisha kasinoma ya seli za msingi
Kasinoma ya seli za msingi mara nyingi husababishwa na kukaa juani.
Dalili za kasinoma ya seli za msingi ni zipi?
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Kasinoma ya seli za msingi kwa kawaida ni uvimbe kwenye ngozi yako (kwa kawaida kwenye kichwa chako au shingo) ambao ni:
Mdogo, unaong'aa, mgumu na ulioinuka
Karibu rangi dhahiri hadi kuwa nyeupe
Imejaa mishipa ya damu midogo inayoonekana
Wakati mwingine, ikiwa na mstari mnene wenye rangi nyeupe
Unaweza pia kuonekana kama:
Uvimbe ulioinuka ambao unaweza kuvunjika na kutengeneza vigaga katikati
Mabaka mekungu au yaliyosawijika yanayoonekana kama makovu
Vidonda vinavyovuja damu, vinatengeneza kigaga na kupona
Uvimbe kwa kawaida hukua polepole lakini unaweza kukua hadi nusu inchi (zaidi ya sentimita 1) kwa mwaka.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kasinoma ya seli za msingi?
Ili kujua ikiwa una aina hii ya saratani ya ngozi, madaktari:
Watachukua kipande cha tishu kwa ajli ya uchunguzi (kuondoa sampuli ndogo ya ngozi na kuichunguza kwenye hadubini)
Je, madaktari wanatibu vipi kasinoma ya seli za msingi?
Ili kutibu kasinoma ya seli za msingi, madaktari wataondoa saratani kwa kutumia njia moja wapo kati ya hizi:
Sugua na uchome kwa sindano ya umeme
Ikate kupitia upasuaji
Angamiza saratani kwa baridi kali (matibabu ya kutumia baridi) au mnururisho
Kuweka dawa za tibakemikali kwenye saratani
Ikiwa saratani imeenea kwenye maeneo mengine ya mwili wako, daktari wako anaweza kukupa tibakemikali kwa njia ya kinywa.
Ninawezaje kuzuia kasinoma ya seli za msingi?
Njia nzuri ya kuzuia kasinoma ya seli za msingi ni kupunguza kukaa kwenye jua:
Jiepushe na jua—kaa kivulini, jaribu kuepuka jua kati ya saa 4:00 asubuhi na saa 10:00 jioni
Usiote jua wala kuingia kwenye mashine ya kufanya ngozi nyeusi
Vaa mavazi ya kujikinga, kama vile mashati ya mikono mirefu, suruali na kofia pana
Tumia mafuta ya kujikinga na jua ambayo yana angalau vipengele 30 vya ulinzi dhidi ya jua (SPF)—ni muhimu kutumia mafuta zaidi ya kuzuia jua kila baada ya saa 2 na baada ya kuogelea au kutokwa jasho
Mwone daktari ukiona mabadiliko ya upele kwenye ngozi baada ya wiki chache.