Kasinoma ya seli ya skwamasi

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2023

Kasinoma ya seli ya skwamasi ni nini?

Kasinoma ya seli ya skwamasi ni aina ya saratani ya ngozi. Inaanzia sehemu ya juu kabisa ya ngozi yako (epidemisi).

  • Kasinoma ya seli ya skwamasi ni saratani ya ngozi inayoshika nafasi ya pili kwa kuenea (baada ya kasinoma ya seli za msingi)

  • Kwa kawaida huwa inakua kwenye ngozi ambayo imekuwa juani, lakini inaweza kukua sehemu yoyote kwenye ngozi au kwenye kinywa

  • Watu wenye ngozi nyeupe wana uwezekano mkubwa wa kuipata kuliko wenye ngozi nyeusi

  • Kwa kawaida kasinoma ya seli ya skwamasi haienei na madaktari wanaweza kutibu saratani hiyo kwa kuiondoa

  • Wakati mwingine saratani hiyo inasambaa kwenda katika sehemu zingine za mwili wako na inaweza kuwa hatari sana

Nini kinachosababisha kasinoma ya seli ya skwamasi?

Kasinoma ya seli ya skwamasi mara nyingi husababishwa na kukaa juani. Ngozi ambayo imeharibika au kujeruhiwa ina uwezekano mkubwa wa kuwa na kasinoma ya seli ya skwamasi.

Dalili za kasinoma ya seli ya skwamasi ni zipi?

Mwanzoni, unakuwa uvimbe kwenye ngozi yako ambao ni:

  • Mnene, mwekundu na wenye magamba

  • Si umbo maalumu

  • Wenye magamba

Uvimbe huu hauponi au kuondoka.

Mifano ya kasinoma ya seli ya skwamasi
Kasinoma ya seli ya skwamasi
Kasinoma ya seli ya skwamasi

Kasinoma ya seli ya skwamasi inaweza kujitokeza kwa njia tofauti. Picha hii inaonyesha ile ambayo imevimba, yenye ukurutu na magamba.

... soma zaidi

Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.

Kasinoma ya Seli ya Skwamasi (Mkono)
Kasinoma ya Seli ya Skwamasi (Mkono)

Sehemu hii nyekundu isiyo ya kawaida kwenye mkono, iligunduliwa kuwa ni kasinoma ya seli ya skwamasi baada ya kuchukua tishu kwa ajili ya uchunguzi.

... soma zaidi

© Springer Science+Business Media

Kasinoma ya Seli ya Skwamasi (Ndewe ya sikio)
Kasinoma ya Seli ya Skwamasi (Ndewe ya sikio)

Kasinoma ya seli ya skwamasi inaweza kujitokeza kwa njia tofauti. Picha hii inaonyesha eneo ambalo lina ukurutu, magamba na nyeusi zaidi kuliko ngozi inayoizunguka. Iligunduliwa kuwa ni kasinoma ya seli ya skwamasi baada ya kuchukua tishu kwa ajili ya uchunguzi.

... soma zaidi

DKT P. MARAZZI/MAKTABA YA PICHA ZA KISAYANSI

Isipotibiwa, uvimbe huo unaweza kuwa:

  • Imetuna, ngumu na yenye usugu

  • Kidonda kilichowazi na kinakuwa na kubadilika kuwa tishu chini yake

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kasinoma ya seli ya skwamasi?

Madaktari watachukua kipande cha tishu kwa ajili ya uchunguzi (kukata kipande kidogo cha sampuli ya ngozi yako ili kuichunguza kwa kutumia hadubini).

Je, madaktari wanatibu vipi kasinoma ya seli ya skwamasi?

Ili kutibu kasinoma ya seli ya skwamasi, madaktari watafanya moja wapo kati ya haya:

  • Sugua na uchome kwa sindano ya umeme

  • Ikate kupitia upasuaji

  • Angamiza saratani kwa baridi kali (matibabu ya kutumia baridi) au mnururisho

  • Weka tibakemikali kwenye saratani

  • Ikiwa saratani imeenea kwenye maeneo mengine ya mwili wako, daktari wako anaweza kutumia tiba ya mionzi

Ninawezaje kuzuia kasinoma ya seli ya skwamasi?

Njia nzuri ya kuzuia kasinoma ya seli ya skwamasi ni kupunguza kukaa kwenye jua:

  • Jiepushe na jua—kaa kivulini, jaribu kuepuka jua kati ya saa 4:00 asubuhi na saa 10:00 jioni

  • Usiote jua wala kuingia kwenye mashine ya kufanya ngozi nyeusi

  • Vaa mavazi ya kujikinga, kama vile mashati ya mikono mirefu, suruali na kofia pana

  • Tumia mafuta ya kujikinga na jua ambayo yana angalau vipengele 30 vya ulinzi dhidi ya jua (SPF)—ni muhimu kutumia mafuta zaidi ya kuzuia jua kila baada ya saa 2 na baada ya kuogelea au kutokwa jasho

Mwone daktari ukiona mabadiliko ya upele kwenye ngozi baada ya wiki chache.