Nyenzo za Mada

Lipoma ni nini?

Lipoma ni za mviringo au uvimbe wa mviringo wenye umbo la yai au mafuta ambayo yanakua chini ya ngozi yako.

  • Si saratani

  • Hazisababishi matatizo yoyote, lakini huenda usipendezwe na jinsi zinakaa

  • Wanawake wana uwezekano mkubwa zaidi kuzipata kuliko wanaume

  • Zinaweza kuwa kila mahali kwenye mwili wako

Lipoma zina uwezekano mkubwa wa kuwa kwenye:

  • Mikono ya mbele

  • Kifua

  • Tumbo

  • Shingo

Dalili za lipoma ni nini?

Lipoma ni uvimbe mwororo chini ya ngozi yako. Unaweza kuhisi zikiwa nyororo au thabiti, lakini si ngumu.

  • Kwa kawaida huwa ndogo kuliko upana wa inchi 3 (sentimita 7.6)

  • Ngozi ya kawaida hufunika uvimbe

  • Kwa kawaida huwa una lipoma moja, lakini baadhi ya watu wana nyingi

  • Kwa kawaida lipoma haisababishi dalili zozote, lakini kwa nadra zinauma kidogo

Madaktari wanatibu lipoma aje?

Kwa kawaida lipoma haihitaji matibabu.

Ikiwa kuna mabadiliko kwa lipoma, daktari wako anaweza kuchukua sehemu yake ili kuikagua chini ya hadubini (uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi).

Ikiwa lipoma zako zinakusumbua, madaktari wanaweza kuziondoa kwa kutumia:

  • Upasuaji

  • Kunyonya mafuta mwilini (unyonyaji wa mafuta mwilini kwa mashine)