Angioma za Buibui

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Angioma ya buibui ni nini?

Angioma ya buibui ni alama ndogo ya wekundu angavu kwenye ngozi ambayo inazungukiwa na mistari nyembamba nyekundu. Mistari hii inaweza kufanana kidogo na buibui mdogo, ambavyo ndivyo jinsi ikapewa jina lake. Haisababishwi na buibui.

  • Angioma za buibui ni mishipa midogo ya damu ambayo imekua zaidi kuliko kawaida

  • Hazina madhara na haziumi au kuwa na mwasho

  • Hauzaliwi ukiwa na angioma za buibui—zinatokea baadaye

  • Kwa kawaida huwa zinaisha zenyewe, lakini madaktari wanaweza kuzitoa kwa kutumia leza au sindano ya umeme

Nini husababisha angioma za buibui?

Kisababishaji cha angioma za buibui hakijulikani, lakini baadhi ya watu wana uwezekano mkubwa wa kuzipata:

  • Watu walio na ugonjwa wa ini, kama vile kirosisi

  • Wanawake ambao ni wajawazito au ambao wanatumia dawa za kuzuia mimba

Angioma za buibui kwenye uso ni za kwaida kwa watu wenye ngozi iliyokwanjuka.

Madaktari hutibu vipi angioma za buibui?

Kwa kawaida hakuna matibabu yanahitajika.

Angioma za buibui ambazo zinatokea wakati wa ujauzito au wakati unatumia dawa za kuzuia mimba kwa kawaida huisha zenyewe takriban mwaka mmoja baada ya kujifungua au kuacha kutumia dawa hizo.

Madaktari wanaweza kutoa angioma za buibui kwa kutumia leza au sindano ya umeme.