Tatizo linaloambatana na saratani ni nini?
Neoplasm ni uvimbe usio wa kawaida katika mwili wako ambao unaweza kuwa na seli za saratani. Ikiwa kitu kinarejelewa kama “neoplastiki,” basi kinahusiana na uvimbe huo. Matatizo ya paraneoplastiki ni mkusanyiko wa dalili zinazosababishwa na saratani. Dalili hizo hutokea katika sehemu tofauti ya mwili wako kando na mahali saratani ilipo.
Watu wengi walio na saratani huwa hawapati tatizo la paraneoplastiki.
Magonjwa ya paraneoplastiki husababishwa na saratani yako kutengeneza homoni au mfumo wako wa kingamwili kutengeneza seli za kingamwili zinazoshambulia tishu za mwili wako (ziitwazo kingamwili otomatiki) zinazosafirishwa na damu yako
Magonjwa ya paraneoplastiki husababisha dalili tofauti kulingana na tishu na ogani zilizoathiriwa
Angalau mtu 1 kati ya watu 5 walio na saratani hupata magonjwa ya paraneoplastiki—mara nyingi hutokea kwa wagonjwa wa saratani ya mapafu
Je, ni zipi dalili za magonjwa ya paraneoplastiki?
Dalili za jumla
Homa
Kutokwa jasho usiku
Kupoteza hamu ya kula
Kupungua uzani
Dalili za ngozi
Kuwasha
Kuiva uso, kunakosababisha uso, shingo, au sehemu ya juu ya kifua kuwa na joto kiasi na kuwa rangi nyekundu
Dalili za kinyurolojia (ubongo, uti wa mgongo, na neva)
Udhaifu au kuishiwa na nguvu
Kupoteza uwezo wa kuhisi
Kutekeleza polepole
Matatizo ya kutumia sehemu mbalimbali za mwili jinsi unavyotaka, kama vile mikono au miguu
Shida ya kuzungumza
Kizunguzungu
Kuona vitu viwili viwili (unapoona vitu 2 badala ya kimoja) au kushindwa kudhibiti mwendo wa macho yako
Saratani inaweza kusababisha dalili hizi bila kubana neva au uti wako wa mgongo.
Dalili za endokrini (mfumo wa homoni)
Udhaifu
Kuongeza uzani
Shinikizo la juu la damu au matatizo ya vali ya moyo
Kuchanganyikiwa
Matatizo ya figo
Ngozi nyekundu na yenye joto
Kuforota
Kuharisha
Dalili nyinginezo
Kuvimba misuli kunakosababisha udhaifu na kuumwa
Kuvimba viungo kwenye maumivu kunakoweza kubadilisha umbo la vidole vya mikono na miguu
Mabadiliko kwenye seli zako za damu (seli nyekundu za damu, seli nyeupe za damu, na chembe sahani)