Kinga Dhidi ya Saratani

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Je, mwili wako hujikinga vipi dhidi ya saratani?

Mfumo wa kingamwili mara nyingi unaweza kupata seli ya saratani na kuiharibu kabla saratani haijakua na kuenea. Mfumo wako wa kingamwili ni mtandao wa seli, tishu na ogani katika mwili wako ambazo husaidia kukulinga dhidi ya magonjwa na maambukizi. Mfumo wako wa kingamwili mara nyingi unaweza kutambua kuwa seli za saratani si za kawaida na uzishambulie.

Kwa nini kinga za mwili hushindwa kudhibiti magonjwa wakati mwingine?

Saratani huenea kwa urahisi zaidi kwa watu walio na mfumo dhaifu wa kingamwili au matatizo kwenye mfumo wao wa kingamwili. Hali hii inaweza kutokea iwapo:

  • Una VVU au UKIMWI

  • Unatumia dawa zinazoweza kupunguza nguvu za mfumo wako wa kingamwili

  • Una zaidi ya miaka 60—kadiri unavyozeeka, ufanisi wa mfumo wako wa kingamwili hupungua

Hata hivyo, hata wakati mfumo wako wa kingamwili unafanya kazi vizuri, wakati mwingine hauwezi kupata na kuharibu seli zote za saratani. Wakati mwingine saratani yako ni kubwa mno hivi kwamba mfumo wa kingamwili hauwezi kuiharibu.