Ugonjwa wa seliaki ni nini?
Chakula hufyonzwa kwenye utumbo wako mdogo. Ugonjwa wa seliaki ni ugonjwa wa kwenye utumbo mdogo unaozuia mwili wako usinyonye virutubishi vyote kwenye chakula chako. Virutubishi ikiwa ni pamoja na protini, wanga, mafuta, vitamini, na madini. Kutofyonza virutubishi kunajulikana kama hali ya kushindwa kunyonya virutubishi. Kutopata virutubushi unavyohitaji huitwa utapiamlo.
Ugonjwa wa seliaki ni ugonjwa wa mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili ambao unarithiwa katika familia.
Unasababisha matatizo kumeng'enya chakula kinachojumuisha gluteni ya protini, ambayo ipo kwenye ngano, shayiri, na vyakula vinavyotengenezwa kutokana na nafaka hizi
Dalili zinajumuisha uharo wenye mafutamafuta unaonuka, kuhisi kuchoka na kupungua uzani
Watoto hawataku kwa kiwango cha kawaida
Hakuna tiba, lakini watu wenye ugonjwa wa seliaki wanaweza kuepuka matatizo kwa kula lishe isiyo na gluteni
Je, nini husababisha ugonjwa wa seliaki?
Ugonjwa wa seliaki ni ugonjwa wa mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili. Mfumo wa kingamaradhi ni mfumo wa ulinzi wa mwili wako ambao unasaidia kukulinda dhidi ya ugonjwa na maambukizi. Ni ugonjwa wa mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili, mfumo wa kingamwili wako hushambulia sehemu za mwili wako mwenyewe.
Katika ugonjwa wa seliaki, mfumo wa kingamaradhi unatoa mjibizo kwenye protini inayoitwa gluteni, ambayo inapatikana kwenye nafaka fulani
Mjibizo wa unatengeneza kingamwili ambayo inaharibu utando wa utumbo wako mdogo
Uharibifu kwenye utando wa utumbo wako unakuzuia kunyonya virutubishi kutoka kwenye chakula
Mafuta ambayo hayajanyinywa yanafanya kinyesi chako kuwa na mafuta
Virutubishi vingine ambavyo vinanyinywa vinaweza kusababisha gesi na kuharisha
Gluteni ni protini iliyo kwenye ngano na kitu chochote kinachotengenezwa kutokana na unga wa ngano. Hiyo ina maana kwamba kuna gluteni kwenye mkate, tambi na vyakula vingi vilivyookwa. Pia kuna kiasi cha gluteni kwenye shayiri. Nafaka nyinginezo kama vile oti, hazina gluteni. Hakuna gluteni kwenye mboga za majani au matunda.
Ugonjwa wa seliaki unarithishwa kwenye familia. Unarithi hali ya kuwa nao. Lakini ni baadhi ya watu kwenye familia ndio tu wanapata ugonjwa huo.
Je, dalili za ugonjwa wa seliaki ni zipi?
Dalili zinaweza kuanza ukiwa mtoto, au huenda zisianze hadi uwe mtu mzima.
Dalili za kawaida zinajumuisha:
Kutohisi njaa
Kuharisha, mara nyingi kinyesi kikiwa na mafuta mafuta
Kuhisi tumbo limejaa na kutoa gesi nyingi
Kujihisi mdhaifu na kupungua uzani
Kwa sababu watoto wanakuwa, wana uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo kutokana na lishe duni. Wataoto wanaweza wasikue kama kawaida na wakawa wafupi na wenye uzani wa chini. Wasichana wanaweza wasipate hedhi wakati walipaswa wapate.
Kushindwa kunyonya vitamini na madini ya kutosha kunaweza kusababisha:
Anemia (kiwango cha chini cha damu)
Vidonda vya mdomo na ulimi uliovimba
Mifupa miembamba inayovunjika kwa urahisi
Hisia za "pini na sindano" (ganzi) kwenye mikono na miguu yako
Dalili zingine ni pamoja na:
Upele unaowasha na kuuma kukiwa na malengelenge madogo (dermatiti ya herpetiformis)
Kuvimba miguu kutokana na majimaji mengi kwenye mwili wako
Matatizo ya kupata ujauzito
Watu wenye ugonjwa wa seliaki wakati mwingine wana matatizo mengine ya mfumo wa kingamaradhi kama vile ugonjwa wa Crohn, kisukari cha aina ya 1, ugonjwa wa tezi dundumio na matatizo mengine ya homoni, na ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa seliaki?
Madaktari hufanya vipimo, ikiwemo:
Kipimo cha damu ili kuangalia kingamwili za gluteni
Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi kutoka kwenye utumbo mdogo
Wakati mwingine, upimaji wa jenetiki
Kwa uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi, madaktari huchukua tishu kwa kutumia ncha za endoskopi (mpira wa kuangalia unaoweza kupinda) na kisha kukagua sampuli hiyo kwa kutumia hadubini.
Je, madaktari wanatibu vipi ugonjwa wa seliaki?
Tiba kuu ni
Kuacha kula chakula chochote chenye glotoni
Hata kiasi kidogo kabisa cha gluteni linaweza kuwa tatizo.
Inaweza kuwa vigumu kuacha kula gluteni. Gluteni si tu ipo kwenye bidhaa za mkate. Ipo kwenye vyakula vingi vilivyosindikwa, ikiwa ni pamoja na baadhi ya supu, michuzi, aisikrimu na mikate. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kula lishe isiyo na gluteni kutoka kwa mtaalamu wa lishe au kikundi cha usaidizi wa seliaki, kama vile Taasisi ya Ugonjwa wa Seliaki.
Ugonjwa wa seliaki pia unakupa uwezekano wa juu wa kupata saratani fulani. Kutokula gluteni kunaweza kupunguza uwezekano huu.
Daktari anaweza kukupa vitamini na madini ili kufidia yale uliyopoteza. Madaktari wanaweza pia kukupa dawa ikiwa una dermatiti ya herpetiformis.