Chakula hufyonzwa kwenye sehemu ya utumbo wako mdogo.
Hali ya kushindwa kunyonya virutubishi ni pale mwili unashindwa kumeng'enya virutubishi katika chakula chako. Virutubishi ni vitu vinavyotosheleza mwili wako. Vinajumuisha protini, wanga, mafuta, vitamini, na madini.
Ugonjwa wa Whipple ni nini?
Ugonjwa wa Whipple ni maambukizi nadra ambayo yanaharibu utando wa utumbo wako mdogo Unapata shida kuvunja (kumeng'enya) chakula na kunyonya virutubishi.
Ugonjwa wa Whipple unaweza kuathiri viungo vingine pia, kama vile moyo wako, mapafu, ubongo, maungio na macho.
Dalili zinaweza kujumuisha kuharisha, maungio yaliyovimba na yenye maumivu, kupungua uzani na maumivu ya tumbo
Dawa za kuua bakteria zinaweza kutibu maambukizi, lakini ugonjwa huo unaweza kurejea tena
Bila matibabu, ugonjwa wa Whipple unaweza kuwa hatari sana
Dalili za ugonjwa wa Whipple ni zipi?
Dalili kuu za ugonjwa wa Whipple ni:
Jointi kuvimba na kupata maumivu
Kuharisha (kinyesi chepesi chenye umajimaji na kinachotoka mara kwa mara)
Maumivu ya tumbo
Kupungua uzani
Dalili zingine ni pamoja na:
Homa
Kutohisi njaa
Anemia (kiwango cha chini cha seli nyekundu za damu), ambayo inaweza kukufanya uwe dhaifu na mchovu
Kikohozi
Vinundu vya limfu vilivyovimba
Ikiwa maambukizi yataenea hadi kwenye ubongo wako—mkanganyiko au kupoteza kumbukumbu
Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nina ugonjwa wa Whipple?
Madaktari wanatambua ugonjwa wa Whipple kwa kutafuta bakteria anayesababisha ugonjwa huo kwenye sampuli ya tishu iliyochukuliwa kwenye utumbo mdogo. Kwa uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi, madaktari huchukua tishu kwa kutumia ncha za endoskopi (mpira wa kuangalia unaoweza kupinda) na kisha kukagua sampuli hiyo kwa kutumia hadubini.
Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa Whipple?
Madaktari wanatibu ugonjwa wa Whipple kwa kutumia dawa za kuua bakteria kwa angalau mwaka mmoja. Wakati mwingine ugonjwa huu unaweza kurejea baada ya kutibiwa.
Ugonjwa wa Whipple usipotibiwa, unakuwa mbaya zaidi na unaweza kuwa hatari.