Muhtasari wa hali ya kushindwa kunyonya virutubishi

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Chakula unachokula kinapaswa kumeng'enywa kabla hakijaupa mwili wako nguvu. Umeng'enyaji unavunja chakula kuwa sehemu mbili tofauti:

  • Protini

  • Fati

  • Kabohaidreti

Protini, fati na kabohaidreti ni virutubishi kwa sababu vinatoa lishe. Virutubishi vingine ni:

  • Vitamini na madini

Chakula kinameng'enywa, virutubisho vinaingia kwenye mwili wako kupitia kuta za utumbo wako. Hali hii inaitwa kunyonya.

Locating the Small Intestine

Hali ya kushindwa kunyonya virutubishi ni nini?

Hali ya kushindwa kunyonya virutubishi humaanisha mwili wako hauchukui vizuri virutubishi (kufyonza) vinavyotoka kwenye chakula Tatizo mahali fulani kwenye njia yako ya mmeng'enyo wa chakula linazuia mwili wako usinyonye aina moja ya virutubishi au zaidi.

  • Hali ya kushindwa kunyonya virutubishi inaweza kusababishwa na magonjwa, upasuaji kwenye utumbo wako, au maambukizi ya utumbo

  • Mara nyingi utapungua uzani na kuharisha na kinyesi kinachonuka (haja kubwa)

  • Baada ya muda unaweza kupata upungufu wa vitamini, hali inayoweza kukupa kiwango cha chini cha damu na kufanya ujihisi kuumwa

  • Madaktari mara nyingi wanafanya vipimo vya kinyesi na damu na wakati mwingine wanaangalia kwenye tumbo na utumbo wako kwa kutumia bomba linalopinda (endoskopia)

  • Visababishi mbalimbali vya hali ya kushindwa kunyonya virutubishi vinahitaji tiba tofauti, lakini madaktari mara nyingi wanajaribu kurekebisha mlo wako ili kuleta unafuu kwenye dalili zako

Nini kinachosababisha hali ya kushindwa kunyonya virutubishi?

Matatizo makuu mawili ndiyo yanasababisha hali ya kushindwa kunyonya virutubishi:

  • Chakula hakimeng'enywi vizuri

  • Utumbo wako hauwezi kunyonya virutubishi

Je, nini kinachosababisha matatizo ya umeng'enyaji wa chakula?

Hutaweza kumeng'enya chakula kikamilifu ikiwa:

Kwa nini huwezi kunyonya virutubishi?

Unapata shida kunyonya virutubishi ikiwa:

Je, dalili za hali ya kushindwa kunyonya virutubishi ni zipi?

Dalili iliyozoeleka sana ya hali ya kushindwa kunyonya virutubishi ni:

  • Hali sugu ya kuhara

Utakuwa na kingi laini chenye mafuta mafumafuta kinachonuka vibaya kuliko kawaida.

Dalili zingine ni pamoja na:

  • Kuhisi tumbo kuwa na gesi na kujaa

  • Kupunguza uzani

  • Kwa wanawake, hedhi kukoma

Upungufu wa vitamini na madini unaweza kusababisha:

  • kiwango cha chini cha damu (anemia)

  • Kuchubuka kwa urahisi

  • Kuwashwa mikono na miguu

Madaktari wanatambuaje hali ya kushindwa kunyonya virutubishi?

Madaktari kawaida hufanya:

  • Vipimo vya kinyesi ili kuangalia mafuta ambayo hayajanyonywa

  • Vipimo vya damu

Ikiwa vipimo hivi vitaonyesha hali ya kushindwa kunyonya virutubishi, basi madaktari watafanya vipimo ili kutafuta kisababishi. Huenda daktari akafanya yafuatayo:

  • Kutazama tumbo na utumbo wako kwa kutumia mawanda ya kutazamia yanayoweza kunyumbulika (uchunguzi wa sehemu za ndani kwa kutumia endoskopi)

  • Fanya kipimo cha kupumua

  • Kufanya kipimo cha eksirei baada ya kumeza majimaji yenye kutofautisha

Je, madaktari hutibu vipi hali ya kushindwa kunyonya virutubishi?

Matibabu yanategemea kisababishi. Baadhi ya magonjwa ya hali ya kushindwa kunyonya virutubishi yana matibabu maalumu. Kwa mfano, sprue ya kitropiki na ugonjwa wa whipple, magonjwa haya yanatibiwa kwa dawa za kuua bakteria.

Kwa ujumla, ikiwa unapata shida kwa kutumia vyakula fulani tu, madaktari watakuambia uviepuke. Ikiwa unakosa vimeng'enya fulani, wakati mwingine unaweza kutumia vidonge vya vimeng'enya. Ikiwa una upungufu wa vitamini, utatumia vitamini vya zaida.