Kuvimba kwa kongosho kali

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024

Kuvimba kwa kongosho kali ni nini?

Kuvimba kwa kongosho ni mwasho (kuvimba) wa kongosho yako. Kongosho yako ni kiungo upande wa juu wa tumbo lako ambacho hutengeneza juisi zinazokusaidia kumeng'enya chakula. Kongosho zako pia hutengeneza insulini, ambayo husaidia kudhibiti sukari yako kwenye damu.

Kuvimba kwa kongosho kwa papo hapo ni kuvimba kwa kongosho ambapo huanza kwa ghafla na kawaida huisha. Kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu kinaitwa kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu.

  • Kwa kawaida, kuvimba kwa kongosho kali kunasababishwa na jiwe la nyongo au kwa kunywa pombe nyingi kwa muda mrefu

  • Kuvimba kwa kongosho kuna viwango toka kiasi hadi hatari zaidi

  • Kuvimba sana kwa kongosho husababisha maumivu makali ya tumbo

  • Madaktari watakutunza kwenye hospitali, hata kama kuvimba kwa kongosho kwako ni kidogo

Kongosho

Ni nini husababisha kuvimba kwa kongosho kali?

Visababishaji vikuu vya kuvimba kwa kongosho kali ni:

Mawe ya nyongo yanaweza kutoka kwenye kibofu nyongo chako na kukwama mahali ambapo mabomba ya mtiririsho wa nyongo kutoka kwenye kibofu nyongo na kongosho huungana. Mawe haya huzuia juisi za utumbo zisitoke kwenye kongosho.

Kunywa pombe kupita kiasi kwa miaka mingi huharibu kongosho yako. Vile unakunywa nyingi na vile unakunywa kwa muda mrefu, ndivyo una uwezekano mkubwa wa kupata kuvimba kwa kongosho.

Kwa wengine wengi, sababu zisizotokea sana za kuvimba kwa kongosho kali zinajumuisha:

  • Matibabu ya dawa au homoni (estrojeni) fulani

  • Viwango vya juu vya mafuta kwenye damu yako

  • Maambukizi ya virusi fulani

  • Jeraha kwenye kongosho yako

  • Saratani kwenye kongosho zako

  • Aina ya kuvimba kwa kongosho ambako unaweza kurithi

Dalili za kuvimba kwa kongosho kali ni zipi?

Dalili kuu ni:

  • Maumivu makali kwenye tumbo yako ya juu ambayo wakati mwingine unahisi pia kwenye sehemu ya katikati ya mgongo wako

Unaweza pia kuwa na dalili kama vile:

  • Kuhisi mgonjwa tumboni na kutapika

  • Kutokwa jasho

  • Moyo unaodunda haraka sana

Ikiwa kuvimba kwa kongosho kwako ni kali sana, unaweza kupata matatizo makali zaidi:

  • Kuharibika kwa viungo vingine vyako, kama vile mapafu au mafigo yako

  • Mshtuko (kupungua sana kwa shinikizo la damu)

  • Maambukizi ya kongosho

  • Kuunda kifuko kilichojawa na kiowevu kwenye kongosho yako (sudosisti)

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kuvimba kwa kongosho kali?

Madaktari hufanya vipimo, ikiwemo:

Daktari wako akishuku mawe ya nyongo, unaweza pia kufanyiwa vipimo vingine kama vile:

  • Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti

  • MRCP (upigaji picha kwa njia ya sumaku wa kolangiopankretografia—aina maalumu ya MRI ambayo huwezesha daktari wako kuona picha za ini, kibofu nyongo, mifereji ya nyongo, kongosho au mfereji wa kongosho)

  • Upigaji picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa kutia mrija (aina maalum ya upigaji picha kwa kutumia mawimbi ya sauti wa kutumia mrija mrefu unaopitishwa mdomoni hadi kwenye utumbo wako)

Je, madaktari wanatibu vipi kuvimba kwa kongosho kali?

Madaktari hutibu kuvimba kwa kongosho kusio kukali kwa kutumia:

  • Kubaki kidogo hospitalini

  • Dawa ya maumivu

  • Majimaji kwenye mshipa wako

  • Ikiwa huwezi kuvumilia vyakula, msaada wa lishe (unapata lishe kupitia kwenye bomba hadi kwenye mshipa wako au kupitia kwenye pua lako na kwenye tumbo au utumbo wako)

Madaktari hutibu vipi kuvimba kwa kongosho hatari kwa kutumia:

  • Kubaki hospitalini

  • Msaada wa Lishe

  • Dawa kwenye mshipa wako kwa maumivu na kuhisi ukiwa mgonjwa

  • Majimaji kwenye mshipa wako

  • Wakati mwingine, bomba kupitia kwenye pua lako hadi kwenye tumbo yako ili kutoa viowevu na hewa

  • Dawa za kupunguza asidi ya tumbo yako

  • Oksijeni au kipumuaji ikiwa uko mgonjwa sana

  • Dawa za kuua bakteria kwa ajli ya maambukizi yoyote

  • Upasuaji ili kuondoa baadhi ya kongosho gonjwa au taratibu zingine ikihitajika, kama vile kufungua mfereji wa kongosho au kutoa jiwe la nyongo