Kuvimba kwa Kongosho kwa Muda Mrefu

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024

Kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu ni nini?

Kuvimba kwa kongosho ni mwasho wa kongosho yako. Kongosho yako ni kiungo upande wa juu wa tumbo lako ambacho hutengeneza juisi zinazokusaidia kumeng'enya chakula. Kongosho zako pia hutengeneza insulini, ambayo husaidia kudhibiti sukari yako kwenye damu.

Kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu ni hali ya muda mrefu. Tishu ya kovu huundwa kwenye kongosho yako na kuendelea kusababisha matatizo. Kuvimba kwa kongosho ambako huanza kwa ghafla kunaitwa kuvimba kwa kongosho kwa ghafla. Kupata kuvimba kwa kongosho kali mara nyingi kunaweza kusababisha kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu.

  • Kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu husababisha maumivu ya tumbo

  • Maumivu yaweza kuwa ya siku zote au yanaweza kutokea na kuisha

  • Kongosho huacha kutengeneza juisi ili kukusaidia kumeng'enya chakula

  • Wakati mwingine kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu huharibu seli ambazo hutengeneza insulini na unapata kisukari

  • Matibabu yanajumuisha kubadilisha lishe yako, kutumia dawa maalum ili kusaidia kumeng'enya chakula, kuepuka kunywa pombe na kunywa dawa za kupunguza maumivu

Kongosho

Je, nini husababisha kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu?

Visababishaji vya kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu vinajumuisha:

  • Matumizi mabaya ya pombe ya muda mrefu, mabaya sana

  • Kuwa na jeni (tabia ya kimwili unayorithi kutoka kwa mzazi) kwa matatizo fulani, kama vile sisti fibrosisi, hali ya kurithi ya kuvimba kongosho au kuvimba kwa kongosho kutokana na mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili

Wakati mwingine hakuna kisababishaji dhahiri.

Je, dalili za kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu ni zipi?

Dalili kuu ni:

  • Maumivu kwenye tumbo lako ya juu (sehemu iliyo chini ya mfupa wako wa kidari)

Maumivu yanaweza kufuata mojawapo ya mitindo kadhaa:

  • Maumivu ambayo huisha au huacha kuuma lakini yanaendelea kurejea

  • Maumivu makali ambayo yanadumu kwa saa kadhaa au hadi siku kadhaa

Unaweza pia kuwa na dalili zingine kama vile:

  • Kinyesi chenye rangi inayong'aa, kinanukia visivyo kawaida, kikubwa

  • Kupoteza uzani na utapiamlo

  • Kiwango cha juu ya sukari kwenye damu inayosababishwa na kisukari

Kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu kunaweza kuongeza hatari ya saratani ya kongosho.

Madaktari wanawezaje kujua kuwa nina kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu?

Madaktari hufanya vipimo fulani, kama vile:

  • Vipimo vya damu

  • Vipimo vya kinyesi ili kuona ikiwa unafyonza chakula chako

  • Eksirei za tumbo yako

  • Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta)

  • MRCP (aina maalum ya MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ambayo huwezesha daktari wako kuona ini, kibofu nyongo, mfereji wa nyongo, kongosho au mfereji wa kongosho)

  • Upigaji picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa kutia mrija (aina maalum ya upigaji picha kwa kutumia mawimbi ya sauti wa kutumia mrija mrefu unaopitishwa mdomoni hadi kwenye utumbo wako)

Je, madaktari hutibu vipi kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu?

Madaktari wanatibu maumivu yaliyosababishwa na kuvimba kwa kongosho kwa muda mrefu kwa:

  • Kukupatia dawa ya maumivu

Watu walio na kuvimba kwa kongosho kali wanaweza kuhitajiwa kusalia hospitalini.

Madaktari hutibu matatizo ya mmeng'enyo yanayosababishwa na kuvimba kwa kongosho kwa kukwambia:

  • Ule milo 4 hadi 5 yenye mafuta kidogo kwa siku

  • Utumie vitu vya kimeng'enya cha kongosho ili kukusaidia kumeng'enya chakula vizuri

  • Wakati mwingine, tumia vitamini fulani (A, D, E, na K)

Madaktari watakwambia uepuke pombe na uache kuvuta sigara.

Unaweza kuhitaji matibabu ya matatizo yanayosababishwa na kuvimba kwa kongosho yako kwa muda mrefu, kama vile dawa au insulini ya kisukari.

Madaktari wanaweza kufanya upasuaji ili kutibu kuvimba kwa kongosho yako kwa muda mrefu ikiwa una maumivu makali na matibabu mengine hayakusaidii. Wanaweza kuondoa baadhi ya kongosho zilizokufa, kufungua mfereji wa kongosho au kukata neva karibu na kongosho ili kutuliza maumivu.