Sprue ya Kitropiki

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Sprue ya kitropiki ni nini?

Sprue ya kitropiki ni tatizo la nadra lenye kuathiri watu walio katika nchi zenye hali ya kitropiki na nusu kitropiki. Husababisha matatizo kwenye utando wa utumbo wako mdogo, mahali ambapo chakula kinafyonzwa. Kisha unapata shida kuvunja (kumeng'enya) chakula na kunyonya virutubishi. Kutofyonza virutubishi kunajulikana kama hali ya kushindwa kunyonya virutubishi.

  • Dalili zinajumuisha kutojisikia vizuri, kinyesi chenye rangi nyeupe, kuharisha na kupungua uzani

  • Daktari anaangalia dalili kwa mtu ambaye anaishi au hivi karibuni alitembelea maeneo ambapo ugonjwa huu unapatikana sana (Kariba, India ya Kusini na Asia ya Kusini Mashariki)

  • Madaktari wanatumia tetracyline (dawa za kuua bakteria) ili kutibu sprue ya kitropiki

Je, nini husababisha sprue ya kitropiki?

Madaktari hawajui kinachosababisha sprue ya kitropiki, lakini wanadhani inaweza kutokana na maambukizi.

Dalili za sprue ya kitropiki ni zipi?

Dalili zinaweza kujumuisha:

  • Kinyesi kikubwa chenye rangi nyeupe, laini, chenye mafuta na mara nyingi kinatoa harufu kali

  • Kuharisha

  • Homa

  • Hisia ya jumla ya kuumwa

  • Kupungua uzani

  • Anemia (kiwango cha chini cha seli nyekundu za damu), ambayo inaweza kukufanya uwe dhaifu na mchovu

Madaktari wanawezaje kujuwa iwapo nina sprue ya kitropiki?

Daktari atahisi kuwa una sprue ya kitropiki endapo:

  • Hivi karibuni uliishi au ulitembelea Kariba, India ya Kusini au Asia ya Kusini Mashariki

  • Una anemia (kiwango cha chini cha seli nyekundu za damu)

  • Kuharisha kwa muda mrefu

Madaktari wanaweza kufanya:

  • Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi kutoka kwenye utumbo mdogo

  • Kupima damu kuangalia utapiamlo

  • Vipimo vya kinyesi ili kuangalia sababu nyingine ya dalili, kama vile, bakteria au vimelea

Kwa kuondoa kipande cha tishu kwa ajili ya uchunguzi, madaktari wanachukua sampuli ndogo ya tishu kwa kutumia vifaa vilivyo mwishoni mwa endoskopi (bomba rahisi la kutazamia). Kisha wanaiangalia sampuli hiyo kwa kutumia hadubidi.

Je, madaktari hutibu vipi sprue ya kitropiki?

Matibabu yanajumuisha:

  • Dawa ya kuua bakteria, tetracycline, wakati mwingine kwa hadi miezi 6

  • Vitamini ili kupata madini chuma ya kutosha, foliti na vitamini B12