Ugonjwa wa Ongezeko la Bakteria

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Ugonjwa wa ongezeko la bakteria ni nini?

Chakula hufyonzwa kwenye utumbo wako mdogo. Bakteria wazuri wanakaa kwenye utumbo wako. Ongezeko la bakteria ni wakati ambapo bakteria wazuri kwenye utumbo mdogo wanaongezeka sana. Bakteria walioongezeka wanakuzuia usinyonye virutubishi vyote kwenye chakula chako. Kutofyonza virutubishi kunajulikana kama hali ya kushindwa kunyonya virutubishi.

  • Bakteria walioongezeka kwenye utumbo wako wanakuzuia usimeng'enye chakula vizuri

  • Bakteria pia wanatumia virutubishi vilivyo kwenye chakula chako ambavyo unavihitaji pia kwa ajili ya afya

  • Baadhi ya watu hawaonyeshi dalili, lakini wengine wanaharisha, wanapungua uzani au wanahisi gesi au tumbo kujaa

  • Madaktari wanaweza kufanya kipimo cha pumzi, kupima sampuli za kiowevu kutoka kwenye utumbo mdogo au kufanya eksirei ya njia ya GI

  • Matadkatari wanatibu ugonjwa wa ongezeko la bakteria kwa kutumia dawa za kuua bakterea na wanaweza kupendekeza ufanye mabadiliko katika mlo wako

Ni kitu gani husababisha ugonjwa wa ongezeko la bakteria?

Ugonjwa wa ongezeko la bakteria hasa husababishwa na:

  • Hali ambazo zinahafifisha njia ya GI, ambazo zinazuia utumbo wako usisafishe bakteria wa ziada

Visababishi vikuu vya kuhafifisha ni:

Magonjwa mengine yanayoweza kusababisha kuhafifisha hujumuisha tezi dundumio isiyofanya kazi vizuri (dudumio lisiloamilifu), sklerosisi ya mfumo, na amiloidosisi.

Aina fulani za upasuaji kwenye utumbo wako na matatizo ya upasuaji pia yanaweza kusababisha bakteria kuongezeka.

Dalili za ugonjwa wa ongezeko la bakteria ni zipi?

Baadhi ya watu wana dalili chache au kupungua uzani tu.

Dalili za kawaida ni:

  • Kuharisha ambapo kinyesi kina mafutamafuta na kinanuka

  • Maumivu ya tumbo

  • Kuvimba tumbo

  • Kutoa gesi kuliko kawaida

  • Baada ya miezi na miaka kadhaa, upungufu wa vitamini na madini

Upungufu wa vitamini na madini unaweza kusababisha:

  • kiwango cha chini cha damu (anemia)

  • Kuchubuka kwa urahisi

  • Kuwashwa mikono na miguu

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa ongezeko la bakteria?

Madaktari wanatambua ugonjwa wa ongezeko la bakteria kulingana na dalili zako na ikiwa una matatizo yanachangia ongezeko la bakteria kwenye utumbo mpana. Wanaweza pia:

  • Kutazama tumbo na utumbo wako kwa kutumia mawanda ya kutazamia yanayoweza kunyumbulika (uchunguzi wa sehemu za ndani kwa kutumia endoskopi)

  • Chukua sampuli ya kiowevu cha kwenye utumbo mdogo kisha kukuza kiowevu hicho ili kupima kiwango cha bakteria

  • Pima kemikali fulani kwenye pumzi yako

  • Kufanya kipimo cha eksirei kwenye tumbo lako baada ya kumeza majimaji yenye kutofautisha

Madaktari wanatibu vipi ugonjwa wa ongezeko la bakteria?

Matibabu yanaweza kujumuisha:

  • Dawa za kuua bakteria

  • Kupunguza kula kabohaidreti na vyakula vya nyuzinyuzi

  • Kutumia vitamini na madini ili kusahihisha upungufu fulani

Watu wengi wanapata nafuu baada ya kutumia dawa za kuua bakteria kwa siku 10 hadi 14.

Madaktari wanaweza kupendekeza ule chakula ambacho kina fati nyingi na kabohaidreti na nyuzinyuzi kidogo ili kupunguza kasi ya ukuaji wa bakteria.