Dundumio lisiloamilifu

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Dundumio yako inapatikana chini ya kongomeo kwenye shingo yako.

Dundumio lako hutengeneza homoni za dundumio. Homoni hudhibiti kasi ya utendakazi wa kemikali za mwili wako (kiwango cha kimetaboli). Karibu kila seli mwilini inahitaji homoni za dundumio. Miongoni mwa majukumu mengine mengi, homoni za dundumio husaidia kudhibiti:

  • Jinsi mwili unavyotumia kalori

  • Jinsi moyo wako unavyopiga haraka

  • Joto la mwili wako

Iodini inahitajika na tezi dundumio ili kutengeneza homoni za dundumio. Unahitaji tu kiasi kidogo cha iodini. Lakini ikiwa tezi dundumio haitapata iodini, haitaweza kutengeneza homoni za dundumio za kutosha.

Kufikia Tezi Dundumio

Dundumio lisiloamilifu ni nini?

Dundumio lisiloamilifu ni pale ambapo dudumio lako halitengenezi homoni za dudumio za kutosha.

  • Dundumio lisiloamilifu ni hali inayowapata sana wanawake watu wazima

  • Ugonjwa unaoitwa Hashimoto thairoditisi ni kisababishi kikubwa

  • Unaweza kuhisi umechoka, uvivu na baridi

  • Dundumio lisiloamilifu mara nyingi huanza taratibu

  • Vipimo vya damu vinaweza kuthibitisha kwamba una dundumio lisiloamilifu

  • Huenda ukahitaji kutumia vidonge vya homoni ya dudumio katika maisha yako yote

Nini husababisha dundumio lisiloamilifu?

Sababu za dundumio lisiloamilifu ni pamoja na:

  • Hashimoto thairoditisi

  • Upasuaji au tiba ya mionzi kuondoa au kusitisha dudumio

  • Upungufu wa iodini

  • Matatizo ya tezi ya pituitari

Ukiwa na ugonjwa wa Hashimoto thairoditisi, mfumo wa kingamaradhi wa mwili wako unashambulia kimakosa dundumio lako. Aina hii ya ugonjwa huitwa ugonjwa wa mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili.

Upungufu wa iodini ni nadra katika nchi zilizoendelea. Nchi nyingi zinaweza iodini kidogo kwenye chumvi hivyo kila mtu anapata ya kutosha. Pia kuna iodini kwenye vyakula vya baharini. Watu katika baadhi ya nchi masikini zilizo mbali na bahari zipo hatarini kukosa iodini ya kutosha.

Tezi ya pituitari katika ubongo wako inatengeneza homoni inayoitwa TSH inayoliambia dudumio lako kutengeneza homoni ya dudumio. Ikiwa una tatizo kwenye tezi ya pituitari, inaweza isitengeneze TSH na utapata dundumio lisiloamilifu.

Je, nani anaweza kupata dundumio lisiloamilifu?

Karibu kila mtu anaweza kupata dundumio lisiloamilifu, lakini huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa. Wakati mwingine, dundumio lisiloamilifu linaweza kutokea kwa:

  • Watoto wachanga waliozaliwa hivi karibuni

  • Wanawake wakati wa ujauzitoo au baada ya ujauzito

  • Watu wenye magonjwa mengine ya mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili kama vile ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi

Dalili za dundumio lisiloamilifu ni zipi?

Kushindwa kutengeneza homoni za dudumio za kutosha kunasababisha shughuli za mwili wako kupungua, jambo ambalo linaweza kuathiri jinsi unavyoonekana, unavyosikika au unavyohisi.

Dalili ambazo zinaathiri vile unavyoonekana au kusikika zinaweza kujumuisha:

  • Macho na uso uliovimba na kope zilizoinama

  • Nywele nyembamba, kavu

  • Ngozi nene ngumu, kavu na yenye magamba

  • Sauti yenye kukwaruza na kuzungumza taratibu

Dalili ambazo zinaathiri vile unavyohisi zinaweza kujumuisha:

  • Kufunga choo

  • Kuhisi baridi haraka

  • Mikono kuuma au kuwa na mchonyoto

  • Mpigo wa moyo wa polepole

  • Mkanganyiko, usahaulifu na mfadhaiko

Usipotibiwa, dundumio lisiloamilifu linaweza kusababisha:

Kwa watu wenye umri mkubwa, mkanganyiko na usahaulifu unaweza kudhaniwa kuwa ni ugonjwa wa Alzheimer au aina nyingine ya kupungua kwa utambuzi.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina dudumio lisiloamilifu?

Madaktari watafanya:

Je, madaktari wanatibu vipi dudumio lisiloamilifu?

Madaktari wanatibu dundumio lisiloamilifu kwa kutumia:

  • Vidonge vya homoni za dundumio

Baada ya kuanza kutumia vidonge, daktari wako atarekebisha dozi taratibu kulingana na kiwango cha TSH yako. Ni muhimu kuzungumza na daktari wako kuhusu dawa zinazoingiliana na kunyonya homoni ya dudumio. Dawa hizi zinajumuisha madini chuma, kalsiamu na baadhi ya dawa za kupunguza asidi.