Hipathiroidi

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024
Nyenzo za Mada

Dundumio lako linapatikana chini ya kongomeo mbele ya shingo lako.

Dundumio lako hutengeneza homoni za dundumio. Homoni hudhibiti kasi ya utendakazi wa kemikali za mwili wako (kiwango cha kimetaboli). Karibu kila seli mwilini inahitaji homoni za dundumio. Miongoni mwa majukumu mengine mengi, homoni za dundumio husaidia kudhibiti:

  • Jinsi mwili unavyotumia kalori

  • Jinsi moyo wako unavyopiga haraka

  • Joto la mwili wako

Locating the Thyroid Gland

Hipathiroidi ni nini?

Hipathiroidi ni pale ambapo dundumio lako linafanya kazi kupita kiasi na linatengeneza homoni za dundumio nyingi zaidi kuliko mwili wako unavyohitaji.

  • Dalili zinajumuisha mapigo ya moyo ya haraka, shinikizo la juu la damu, na kupungua uzani

  • Kipimo cha damu kinaweza kuthibitisha una hipathiroidi

  • Dawa zinaweza kusaidia kutibu hipathiroidi

  • Hipathiroidi hutokea karibu kwa mtu 1 kati ya watu 100

Dhoruba ya dundumio ni hipathiroidi kali sana ambayo inatokea wakati dundumio lako linatoa kwa ghafula kiwango hatarishi cha homoni. Kwa kawaida inasababishwa na maambukizi, shambulio la moyo, kiharusi, upasuaji, na msongo mkubwa sana. Ni dharura ambayo inaweza kusababisha kifo ikiwa haitatibiwa haraka.

Hipathiroidi husababishwa na nini?

Sababu kuu ni pamoja na:

  • Ugonjwa wa Graves

  • Kuvimba kwa dundumio (thairoditisi)

  • Uvimbe (vifundo) kwenye dundumio lako

  • Dawa fulani

Ukiwa na ugonjwa wa Graves, mfumo wa kingamaradhi wa mwili wako unashambulia kimakosa dundumio (ugonjwa wa mfumo wa kinga kwenda kinyume na mwili). Magonjwa mengi ya mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili yanafanya vitu viache kufanya kazi. Lakini katika ugonjwa wa Graves, mashambulizi yanayofanywa na mfumo wa kingamaradhi hufanya dudumio lako kufanya kazi sana na kutengeneza homoni zaidi za homoni ya dudumio.

Thairodititisi hutokana na maambukizi fulani ya virusi na magonjwa mengine ambayo yanafanya dudumio lako livimbe. Seli zilizoharibika kwenye dudumio lililovimba zinaweza kuzalisha homoni za dudumio za ziada.

Vinundu vya dudumio ni vinyama vidogo ambavyo mara nyingi vinatokana na ugonjwa wa vinasaba. Baadhi ya vinundu hutoa homoni za dudumio. Saratani za dudumio pia ni vinyama vidogo, lakini vinazalisha kwa nadra homoni za dudumio.

Zipi ni dalili za hipathiroidi?

Dalili za hipathiroidi kwa kawaida zinahusisha kuharakisha shughuli za mwili. Kwa hivyo unaweza kuwa na:

  • Shinikizo la juu la damu

  • Mapigo ya moyo ya haraka na moyo kudunda haraka sana (hali ya mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida)

  • Kutokwa jasho sana na hisia za kuwa wa moto sana wakati wote

  • Mikono inayotetemeka

  • Woga, hofu na kupata shida kulala

  • Kupungua uzani

  • Kujisadia mara kwa mara, wakati mwingine ukipatwa na hali ya kuharisha

  • Kwa wanawake, hedhi isiyo ya kawaida au isiwepo kabisa

Baadhi ya magonjwa ambayo yanasababisha hipathiroidi hufanya tezi dudumio kuvimba au kuuma.

Watu wenye umri mkubwa wenye hipathiroidi wanaweza kuwa na dalili chache zilizo dhahiri. Dalili kwa watu wenye umri mkubwa zinaweza kujumuisha:

  • Udhaifu

  • Kuchanganyikiwa

  • Kupungua uzani

  • Mfadhaiko

Watu wenye ugonjwa wa Graves wanaweza kuwa na matatizo kwenye macho yao ikiwa ni pamoja na:

  • Macho yenye uvimbe

  • Macho mekundu

  • Macho makavu

  • Wakati mwingine, uoni hafifu au kuona vitu viwiliviwili

Dhoruba ya dundumio

Dalili za dhoruba ya dundumio ni sawa na zile za hipathiroidi ya kawaida lakini ni kali zaidi, ikiwa ni pamoja na:

  • Homa kali

  • Uchovu kupita kiasi

  • Wasiwasi na kuchanganyikiwa

  • Kuzirai

  • Mshtuko (shinikizo la damu kushuka sana)

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina hipathiroidi?

Madaktari watafanya:

Je, madaktari wanatibu vipi hipathiroidi?

Matibabu yanategemea kilichosababisha hipathiroidi.

Madaktari watakutibu kwa:

  • Dawa, kama vile vizuizi vya beta, ili kudhibiti dalili

  • Dawa za kufanya dudumio lako lisitengeneza homini za dudumio

Wakati mwingine, madaktari wanatakiwa kuisitisha kabisa thairodi yako isitengeneze homoni zaidi. Wanaweza kusitisha dudumio lako kwa:

  • Kufanya upasuaji ili kuondoa sehemu au dudumio lako lote

  • Kukupatia dozi kubwa ya iodini ya mionzi, ambayo itaharibu dudumio

Baada ya kufanyiwa upasuaji au kupewa matibabu ya iodini ya mionzi, utapaswa kutumia vidonge vya homoni ya dudumio kwa sababu mwili wako hautengenezi tena homoni za dudumio.