Muhtasari wa Tezi ya Pituitari

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023
Nyenzo za Mada

Tezi ya pituitari ni nini?

Tezi ya pituitari ni kipande cha tishu chenye ukubwa wa kunde kinachopatikana chini ya ubongo. Tezi ni viungo vinavyotengeneza na kutoa homoni kwenye damu. Homoni ni kemikali zinazochochea seli au tishu nyingine kufanya kazi. Tezi ya pituitari hutoa homoni nyingi tofauti. Kila homoni ya pituitari inadhibiti tezi tofauti na kazi ya mwili.

Tezi ya pituitari inadhibitiwa na sehemu ya ubongo inayoitwa hipotalamu.

Kufikia Tezi ya Pituitari

Homoni za pituitari ni nini?

Kila homoni ya pituitari hudhibiti tezi na shughuli mbalimbali za mwili.

Homoni za pituitari hujumuisha:

  • ACTH (homoni ya adrenocorticotropic): Hudhibiti homoni zako za tezi ya adrenali, ambazo huathiri kipimo cha mapigo ya moyo, shinikizo la damu, na usawa wa chumvi na maji katika mwili wako.

  • Homoni za ukuaji: Hudhibiti kasi na kiwango cha kukua kwa mwili wako

  • Homoni ya kuchochea dundumio: Hudhibiti homoni zako za tezi dundumio, ambazo hudhibiti kiwango cha kasi ya utendakazi wa shughuli za kemikali za mwili wako (kiwango cha umetaboli)

  • Homoni ya lutein na homoni ya kuchochea foliko: Hudhibiti homoni zako za ngono tesistosteroni na estrojeni, ambazo huathiri uzazi

  • Prolaktini: Hudhibiti uzalishaji wa maziwa kwenye matiti

Je, nini hutokea ikiwa tezi yako ya pituitari haifanyi kazi vizuri?

Tezi yako ya pituitari inaweza:

  • Isitengeneze homoni za kutosha

  • Ikatengeneza homoni nyingi kupita kiasi

Wakati mwingine kuna tatizo na homoni moja pekee ya pituitari. Nyakati nyingine, homoni kadhaa au zote huwa na tatizo.

Iwapo tezi yako ya pituitari itazalisha homoni kwa kiasi kikubwa, au kiasi ambacho hakitoshi, unaweza kupata matatizo ya kiafya kama vile:

Je, nini husababisha matatizo ya tezi ya pituitari?

Sababu za matatizo ya tezi ya pituitari ni pamoja na:

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina matatizo ya tezi ya pituitari?

Madaktari hushuku uwepo wa matatizo ya tezi ya pituitari kutokana na dalili zako. Atafanya vipimo kama vile:

  • Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) au MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ya ubongo ili kuona kama tezi yako ya pituitari imeongezeka au kusinyaa

  • Vipimo vya damu vinavyopima viwango vya homoni zitokazo kwenye tezi ya hipotalamu, pituitari na tezi nyinginezo

Je, madaktari wanatibu vipi matatizo ya tezi ya pituitari?

Tiba inategemea aina ya tatizo ulilonalo. Inaweza kujumuisha:

  • Dawa ya kuzuia athari za kiwango kikubwa cha homoni

  • Upasuaji ili kuondoa uvimbe

  • Tiba ya homoni ili kurudishia zile homoni ambazo mwili wako hauzitengenezi kwa kiasi kinachotosha