Kisukari Kisichosababishwa na Insipidus ya Kati

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Kisukari Kisichosababishwa na Insipidus ya Kati ni nini?

Kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati ni hali ya kutokuwa na homoni ya kutosha inayoitwa vasopressini. Homoni ni kemikali zinazochochea seli au tishu nyingine kufanya kazi. Vasopressini ni homoni inayotoa ishara kwa figo zako ili ziunde kiasi kidogo cha mkojo ili mwili wako uweze kuhifadhi maji. Vasopressini huundwa katika sehemu ya ubongo wako inayoitwa hipotalamu na kisha kuhifadhiwa na kuachiliwa kutoka kwenye tezi ya pituitari. Hipotalamu na pituitari zote zinapatikana chini ya ubongo wako.

  • Kuwa na viwango vya chini vya vasopressini hukufanya ukojoe mara nyingi hivyo unapata kiu sana

  • Kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati mara nyingi husababishwa na tatizo kwenye ubongo, kama vile uvimbe au jeraha, au upasuaji kwenye ubongo

  • Madaktari hupima mkojo na damu baada ya wewe kumaliza kiasi cha saa 12 pasipo kunywa maji

  • Kwa kawaida madaktari hutibu kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati kwa kutumia kinyunyizio cha puani cha vasopressini

Kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati ni tofauti na ugonjwa wa kawaida unaoitwa kisukari, ambapo kiwango cha sukari kwenye damu yako huwa cha juu sana. Ugonjwa huo wa sukari kwenye damu ni ugonjwa wa sukari Mbali na kukufanya ukojoe sana, kisukari kisichosababishwa na insipidus hakina uhusiano wowote na ugonjwa wa sukari.

Je, nini husababisha kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati?

Sababu za kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati hujumuisha:

  • Uharibifu wa bahati mbaya wa tezi yako ya pituitari wakati wa upasuaji

  • Jeraha kwenye ubongo, hasa kuvunjika kwa sehemu ya chini ya fuvu

  • Kivimbe kwenye ubongo

  • Sakroidosisi

  • Kifua kikuu

  • Damu kuzuiwa kutiririka kwenye ubongo wako

  • Kuvimba kwa ubongo (ubongo kuvimba kwa sababu ya maambukizi)

Zipi ni dalili za kisukari kisichosababishwa na insipidusi ya kati?

Dalili za kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati ni pamoja na:

  • Kiu kupita kiasi, hasa kwa maji baridi yenye barafu—baadhi ya watu hunywa hadi galoni 10 kwa siku

  • Kukojoa kila mara (pamoja na kuamka ili kukojoa nyakati za usiku)

Ikiwa huna maji ya kutosha mwilini mwako, unaweza kukosa maji mwilini. Hii inaweza kusababisha shinikizo la chini la damu ambalo ni hatarishi.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati?

Madaktari hupima uwepo wa kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati kwa kutumia:

  • Vipimo vya mkojo

  • Vipimo vya damu

Madaktari hufanya vipimo vya damu na mkojo wakati ambapo hujanywa maji yoyote. Unaweza kumaliza hadi saa 12 bila kunywa maji (kipimo cha kujinyima maji). Ikiwa utaendelea kukojoa licha ya kutokunywa chochote, unaweza kuwa na kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati. Kisha madaktari hukuchoma sindano ya vasopressini na kuangalia namna mwili wako utakavyoitika.

Je, madaktari wanatibu vipi kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati?

Madaktari hutibu kisukari kisichosababishwa na insipidus ya kati kwa kutumia mojawapo ya haya yafuatayo:

  • Kinyunyizi cha pua chenye desmopressini (aina ya vasopressini inayofanya kazi kwa muda mrefu)

  • Dawa ya kuusaidia mwili wako kuunda vasopressini