Upungufu wa teziubongo

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Tezi ya pituitari ni kipande cha tishu chenye ukubwa wa kunde kinachopatikana chini ya ubongo. Tezi ni viungo vinavyotengeneza na kutoa homoni kwenye damu. Homoni ni kemikali zinazochochea seli au tishu nyingine kufanya kazi. Tezi ya pituitari hutoa homoni nyingi tofauti. Kila mojawapo hudhibiti tezi za nyenzake na utendakazi wa mwili.

Kufikia Tezi ya Pituitari

Upungufu wa gonadi ni nini?

Upungufu wa teziubongo hutokea wakati tezi yako ya pituitari inaposhindwa kutengeneza kiasi cha kutosha cha homoni moja au zaidi za pituitari.

  • Upungufu wa teziubongo hautokei mara kwa mara

  • Chanzo cha upungufu wa teziubongo ni pamoja na uvimbe kwenye tezi yako ya pituitari, upungufu wa usambazaji wa damu kwa tezi yako ya pituitari, au magonjwa fulani

  • Mara nyingi dalili huanza polepole na kwa muda mrefu na hutofautiana kulingana na ni homoni gani ambazo ni pungufu

  • Madaktari hutibu chanzo cha hypopituitarism na kukupatia dawa za kuongeza viwango vya homoni zako

Je, nini husababisha upungufu wa teziubongo?

Vyanzo vya teziubongo ni pamoja na:

Wakati mwingine kuna tatizo na homoni moja pekee ya pituitari. Nyakati nyingine, homoni kadhaa au zote huwa na tatizo.

Zipi ni dalili za upungufu wa teziubongo?

Kwa kawaida dalili huanza kidogo kidogo. Dalili ulizonazo hutegemea homoni ulizo na upungufu nazo.

Dalili zinaweza kujumuisha:

  • Kwa watoto, kushindwa kukua

  • Kwa wanawake, kukosekana kwa vipindi vya hedhi na hali ya ukavu kwenye uke

  • Kwa wanaume, kusinyaa kwa korodani na upungufu wa nguvu za kiume

  • Kuchanganyikiwa, kuongezeka uzani na kufunga choo

  • Udhaifu, upungufu wa sukari kwenye damu, na kufadhaika

  • Kushindwa kuzalisha maziwa ya mama baada ya kujifungua mtoto

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina upungufu wa teziubongo?

Madaktari wanaweza kutilia shaka uwepo wa upungufu wa teziubongo pale unapokuwa na shida ya tezi nyingine, kama vile tezi dundumio. Atafanya vipimo, kama vile:

  • Kipimo cha damu ili kupima viwango vya homoni zako

  • Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) au MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ya ubongo ili kuona kama kuna mabadiliko ya pituitari yako

  • Wakati mwingine, vipimo vya kuchunguza mtiririko wa damu kwenda kwenye pituitari yako

Je, madaktari wanatibu vipi upungufu wa teziubongo?

Madaktari hutibu upungufu wa teziubongo kwa:

  • Kutibu chochote kinachosababisha upungufu wa teziubongo wako (kwa mfano, upasuaji au mionzi ya kuondoa au kuharibu uvimbe wa pituitari)

  • Kurudishia homoni ambazo pituitari yako haizitengenezi kwa kiasi kinachotosha