Mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma ni nini?

Mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma ni mifumo ya ukuaji usio wa kawaida unaosababishwa na kuwa na homoni nyingi za ukuaji.

Kwa watoto, homoni nyingi za ukuaji husababisha mwili mkubwa kupita kiasi, ikimaanisha kuwa mrefu mno au pandikizi la mtu.

Kwa watu wazima, homoni nyingi za ukuaji huasababisha kuendelea kukua bila kukoma.

  • Kwa mwili kuwa mkubwa kupita kiasi, watoto hukua na kuwa warefu sana

  • Kwa kuendelea kukua bila kukoma, watu wazima hawaongezeki urefu (kwa sababu eneo la ukuaji kwenye mifupa yao limefungwa), lakini huwa na mifupa na fuvu lenye kasoro

  • Dalili zingine ni pamoja na udhaifu, matatizo ya kuona, na matatizo ya moyo ambayo yanaweza kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi

  • Madaktari hutibu tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma kwa njia ya upasuaji na dawa za kupunguza viwango vya homoni za ukuaji

Je, nini husababisha tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma?

Tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma mara nyingi husababishwa na:

  • Uvimbe usio na kansa (tulivu) au tezi ya pituitari ambayo inazalisha ziada ya homoni ya ukuaji

Tezi ya pituitari ni kipande cha tishu chenye ukubwa wa kunde kinachopatikana chini ya ubongo. Tezi ni viungo vinavyotengeneza na kutoa homoni kwenye damu. Homoni ni kemikali zinazochochea seli au tishu nyingine kufanya kazi. Tezi yako ya pituitari kutengeneza aina mbalimbali za homoni, ikijumuisha homoni ya ukuaji.

Ziada ya homoni ya ukuaji kwenye damu husababisha mifupa, misuli na ogani zako kuongezeka ukubwa

Kufikia Tezi ya Pituitari

Zipi ni dalili za tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi?

Tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi ni ugonjwa wa watoto. Dalili zinajumuisha:

  • Ukuaji uliopita kiasi wa mifupa mirefu, hivyo mikono na miguu hurefuka sana

  • Kurefuka sana

  • Kuchelewa kubalehe kuliko kawaida

  • Wakati mwingine, tatizo la kukua kwa sehemu za siri

Zipi ni dalili za tatizo la kuendelea kukua bila kukoma?

Tatizo la kuendelea kukua bila kukoma ni ugonjwa ambao kwa kawaida huanza kati ya umri wa miaka 30 hadi 50. Tofauti na mifupa ya watoto, mifupa ya watu wazima haiwezi kuongezeka urefu. Badala yake, mifupa yao hubadilika umbo na kuwa na kasoro. Dalili zinajumuisha:

  • sifa za uso mpana, wenye kukwaruza

  • Mikono na miguu iliyovimba

  • Hitaji la kupata pete, glavu, kofia na viatu vyenye saizi kubwa

  • Ubavu mnene wenye umbo la pipa

  • Maumivu ya viungo

  • Wakati mwingine, udhaifu wa miguu na mikono

  • Kwa wanawake, hedhi isiyo ya kawaida

  • Kwa wanaume, upungufu wa nguvu za kiume

Ni matatizo gani husababishwa na mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma?

Tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma lilsipotibiwa linaweza kusababisha:

Watu wenye tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma huwa wana muda mfupi wa kuishi.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi na kuendelea kukua bila kukoma?

Kawaida ni rahisi kuona wakati watoto wanakua sana. Lakini wa watu wazima, inaweza kuchukua muda mrefu kugundua ukuaji wa mifupa usio wa kawaida kwa kuendelea kukua bila kukoma kwa sababu hutokea kidogo kidogo.

Ikiwa madaktari watatilia shaka uwepo wa tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi au kuendelea kukua bila kukoma:

  • Wakati mwingine, watatazama picha zako ulizopigwa kwa muda mrefu—hizi zinaweza kuonyesha mabadiliko ya kimwili ambayo ni ya kawaida kwa tatizo la kuendelea kukua bila kukoma

  • Kipimo cha damu ili kupima viwango vya homoni za ukuaji

  • Kupiga eksirei ya mikono yako ili kuona kama kuna mifupa iliyonenepa au tishu zilizovimba

  • Kufanya uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) au MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ya ubongo ili kuona kama kuna uvimbe kwenye tezi yako ya pituitari

Je, madaktari wanatibu vipi tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi au kuendelea kukua bila kukoma?

Madaktari hutibu tatizo la mwili mkubwa kupita kiasi au kuendelea kukua bila kukoma kwa kutumia mchanganyiko wa:

  • Upasuaji wa kuondoa uvimbe wa tezi ya pituitari

  • Tiba ya mionzi

  • Dawa ambayo hukuzuia kuzalisha homoni ya ukuaji

Baada ya upasuaji au mionzi ya kutibu uvimbe wa tezi ya pituitari, unaweza kutakiwa kutumia homoni za ziada ili kurudishia zile ambazo hutengenezwa na pituitari