Upungufu wa nguvu za kiume ni nini?
Upungufu wa nguvu za kiume (ED) ni wakati mwanamume ana matatizo ya kupata au kushika mshipa (kusimamishwa). Uume wako unaweza usisimame kabisa au mara mojamoja tu baada ya muda fulani. Au unaweza kuusimamisha, lakini haudumu kwa muda wa kutosha.
Ni kawaida kwa wanaume kuwa na matatizo ya kusimamisha mara mojamoja baada ya muda fulani—madaktari hawaoni kuwa ni ED isipokuwa inapotokea mara kwa mara.
ED inaweza kusababishwa na majeraha, matatizo ya kisaikolojia, magonjwa ya mfumo wa neva na mishipa ya damu, dawa fulani, na upasuaji
ED hutokea hasa kwa wanaume wa zaidi ya miaka 40
ED kwa kawaida inatibika
Wakati mwingine ED ni ishara ya matatizo makubwa zaidi ya kiafya.
Muone daktari mara moja ikiwa una ED na:
Unahisi ni kama eneo kati ya miguu yako limekufa ganzi (gongo lako)
Kufa ganzi pamoja na ED inaweza kuwa ishara ya tatizo kwenye uti wa mgongo wako.
Muulize daktari wako ni lini unapaswa kuchunguzwa ikiwa:
Kamwe huwezi kusimamisha usiku au unapoamka asubuhi
Kukakamaa kwa misuli ya miguu yako baada ya mazoezi ambayo huondoka unapopumzika
Ni nini husababisha kutoweza kusimamisha?
Mara nyingi, ED husababishwa na matatizo ya mtiririko wa damu kwenye uume wako au matatizo ya mishipa ya uume wako.
Visababishi vya kawaida vya ED ni:
Ateri katika mwili wako kuwa ngumu (atherosklerosisi)
Madhara kutokana na upasuaji wa tezi dume
Kutumia dawa fulani (hasa dawa za shinikizo la juu la damu au mfadhaiko)
ED pia inaweza kusababishwa na:
Viwango vya chini vya testosteroni
Dawa za kulevya kama vile pombe au kokeni
Mfadhaiko, wasiwasi, unyogovu, au uchovu kupita kiasi
Magonjwa yanayoathiri neva, kwa mfano, kiharusi, sklerosisi ya sehemu nyingi, na kujeruhiwa kwa uti wa mgongo
Je, nitarajie nini ninapokwenda kumwona daktari wangu?
Daktari wako atafanya:
Pima damu yako ili kuchunguza kiwango cha testosteroni na utafute kisukari au matatizo mengine.
Wakati mwingine, fanya atrasonografia ili kuangalia mtiririko wa damu kwenye uume wako
Madaktari hutibu vipi tatizo la nguvu za kiume?
Kwanza, madaktari:
Watatibu matatizo yoyote ya kiafya uliyo nayo ambayo yanaweza kusababisha ED
Wanaweza kubadilisha dawa yoyote unayotumia ambayo husababisha ED
Daktari wako pia anaweza kukushauri:
Punguza uzani
Kuacha kuvuta sigara
Kunywa pombe kiasi
Walakini, matibabu kuu ya ED ni dawa. Kawaida, madaktari huagiza:
Vidonge, kama vile sildenafil (Viagra)
Vidonge kama sildenafil huitwa vizuizi vya phosphodiesterase. Humezwa takriban saa moja kabla ya kufanya ngono. Hupaswi kumeza tembe hizi ikiwa pia unatumia aina fulani ya dawa ya moyo inayoitwa nitrati. Nitrati kama vile nitrogliserini ni dawa za maumivu ya kifua.
Ikiwa huwezi kutumia vizuizi vya phosphodiesterase, daktari wako anaweza:
Kuagiza dawa inayodungwa kwenye uume wako kabla ya ngono
Kuagiza dawa inayowekwa kwenye tundu la uume wako kabla ya ngono
Kuagiza utumie kifaa cha kuvuta
Kifaa cha kuvuta ni bomba la plastiki la duara ambalo unaweka juu ya uume wako. Kina pampu ya mkono ambayo unatumia kuvuta hewa. Huku hukuwezesha kusimamisha.kusisimka. Baada ya kusimka, utaweka pete au mkanda kwenye sehemu ya chini ya uume wako ili uume wako uendelee kusimama unapoondoa pampu.
Ikiwa una ED kali na matibabu haya yote yakose kufanya kazi, madaktari wanaweza:
Kufanya upasuaji kuweka kifaa kwenye uume wako
Kifaa hiki kinaweza kuwa fito thabiti ya silikoni ambayo husimamisha uume wako ukiwa mgumu kila wakati. Au inaweza kuwa kifaa kinachoweza kuvuta hewa ambacho unasukuma ili kusimamisha uume.