Sklerosisi ya Sehemu Nyingi (MS)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2024

Sklerosisi ya Sehemu Nyingi (MS) ni nini?

Sklerosisi ya sehemu nyingi ni ugonjwa ambao unasababisha alama kwenye neva kwenye ubongo na uti wa mgongo wako. Makovu haya huzuia neva kufanya kazi inavyofaa.

  • Unaweza kuwa na matatizo ya kuona, hisia za ajabu, mwendo usio stadi au dhaifu au tatizo katika kufikiria vizuri

  • Utakuwa na dalili tofauti katika nyakati tofauti

  • Kwa kawaida dalili huja na kuisha, na unaweza kuhisi kuwa vizuri kati ya vipindi vya dalili

  • MS huwa mbaya zaidi kwa baada ya wakati

  • Utambuzi unatokana na MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ya ubongo na uti wa mgongo.

  • Dawa tofauti kadhaa zinaweza kusaidia, lakini hakuna tiba

  • MS inaweza kusbabisha ulemavu, lakini watu wengi wana maisha ya kawaida

Ni nini husababisha MS?

Madaktari hawajui ni nini husababisha MS. Lakini madaktari wengi wanaamini kuwa mfumo wako wa kingamwili huvamia tishu za mwili wako wenyewe ni kama si zako. Huu unaitwa mmenyuko wa mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili. Katika MS, mfumo wa kingamwili hushambulia na kuharibu neva kwenye ubongo na uti wa mgongo.

Dalili za MS ni zipi?

Kwa sababu MS huvamia neva tofauti, dalili ni tofauti kwa watu tofauti. Na mkondo wa jinsi dalili huja na kuisha ni tofauti.

Kwa kawaida, dalili za MS hutokea kwa ghafla (inaitwa tanuka) na kisha huisha (kupungua). Kwa kawaida, uko na afya njema kati ya mtanuko. Watu wengi wana mtanuko baada ya mwaka au miwili pekee, lakini wanaweza kuwa na zaidi. Kila mtanuko unaweza kuathiri sehemu tofauti ya mwili wako. Mitanuko inaweza kudumu siku chache hadi miezi chache.

Vile wakati unapita, dalili zako zinaweza isha kabisa kati ya mitanuko. Kwa baadhi ya watu, dalili haziishi kamwe. Chochote mfano wa dalili yako, MS huwa mbaya zaidi polepole.

Dalili za mapema za kawaida za MS zinajumuisha:

  • Kuwashwa au kufanya ganzi katika sehemu za mikono, miguu, kifua, mgongo au uso wako

  • Udhaifu, kutokuwa stadi au ugumu kwenye mikono au miguu yako

  • Sehemu ya mboni isiyoona, uoni hafifu au maumivu unaposongesha jicho moja

Dalili zingine za mapema zinajumuisha:

  • Kuona vitu pacha (kuona vitu mbili vya kitu moja)

  • Maumivu yanayokaa ya mshtuko wa umeme au mwasho chini kwenye mgongo, miguu au mkono wako ambayo yanaweza kutokea yenyewe, wakati kitu kinakugusa au wakati unainamisha shingo yako

Dalili za baadaye ya MS zinaweza kujumuisha:

  • Mwendo usio wa kawaida, kutikisika

  • Kushindwa kusogeza sehemu au mwili wako wote

  • Mikakamao chungu ya misuli na udhaifu wa misuli

  • Ugumu wa kutembea na kuwa wima

  • Kuhisi uchovu na udhaifu

  • Mtamshi yasiyo laini, ya polepole

  • Mfadhaiko au mabadiliko ya hisia

  • Ugumu katika kufikiria, kukumbuka vitu, kuwa makini au kufanya maamuzi

  • Kizunguzungu

  • Matatizo katika kudhibiti kutoa mkojo (kukojoa) au kujisaidia (kutoa kinyesi)

Dalili zinaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa una joto jingi, kama vile kwa siku yenye joto au wakati wa homa.

Madaktari wanawezaje kujua kama nina MS?

Huenda ikawa vigumu kubaini ikiwa una MS. Madaktari hutambua MS kulingana na dalili zako na kwa kawaida kwa:

Madaktari hutibu vipi MS?

Ili kutibu mitanuko ya dalili, madaktari hutumia:

  • Dawa zinaitwa kotikosteroidi

Ikiwa kotikosteroidi hazisaidii, madaktari wanaweza kujaribu matibabu ya damu yanayoitwa ubadilishaji wa plazma.

Ili kusaidia kuzuia mtanuko wa dalili, madaktari hutumia dawa tofauti mbalimbali ambazo husaidia kuzuia mfumo wako wa kingamwili usivamie neva zako.

Madaktari wanaweza kutumia dawa kutibu dalili mahususi, kama vile kubana kwa misuli, hisia za mwasho, uchovu na msongo wa mawazo.

Unaweza kufanya maisha kwa MS rahisi zaidi na kusaidia kuzuia ulemavu kwa:

  • Kuwa amilifu

  • Kufanya matibabu ya kimwili

  • Kutembea peke yako kwa muda mrefu iwezekanavyo

  • Kuepuka joto, kama vile kuoga na maji moto au shawa

  • Kutovuta sigara

  • Kutumia virutubishi vya vitamini D

Ni wapi ninaweza kupata maelezo kuhusu MS?