Je, mfadhaiko ni nini?

Mfadhaiko huzuni au kuhisi goigoi sana hivi kwamba huwezi kufanya majukumu ya kila siku au kushiriki katika shughuli unazozifurahia.

  • Ni kawaida kuhisi huzuni baada ya kitu cha kuhuzunisha kufanyika, kama vile kifo au kupoteza mpendwa—mfadhaiko ni wakati huzuni hiyo si ya muda mfupi na inaendelea zaidi ya kipindi cha muda cha kueleweka

  • Tatizo la mfadhaiko ambalo halijatibiwa hukaa kwa takribani miezi 6, lakini linaweza kuendelea kwa miaka 2 au zaidi

  • Mfadhaiko ndio tatizo la 2 la afya ya akili linalotokea sana, baada ya wasiwasi

  • Wanawake wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa wa mfadhaiko kuliko wanaume

  • Kwa watu wazee, mfadhaiko wnaweza kusababisha dalili zinazofanana na ulegevu wa akili

  • Ugonjwa wa mfadhaiko unaweza kuanza katika umri wowote, ikijumuisha utotoni, lakini kwa kawaida huanza ukiwa kijana au katika miaka ya 20 au 30

  • Madaktari hutibu mfadhaiko kwa dawa za kuzuia msongo wa mawazo (dawa za kutibu mfadhaiko) na usaidizi wa ushauri nasaha (matibabu ya kisaikolojia)

Nenda hospitalini mara moja au upige simu ili upate usaidizi wa matibabu ya dharura (nchini Marekani, piga simu kwa 911) ikiwa wewe au mtu unayemjua anafkiria kujiua.

Nini husababisha mfadhaiko?

Madaktari hawajui haswa kinachosababisha ugonjwa wa mfadhaiko. Una uwezekano mkubwa wa kupata mfadhaiko iwapo:

  • Una wanafamilia ambao wamewahi kuwa na mfadhaiko au ambao wana mfadhaiko

  • Wewe ni mwanamke—viwango vya homoni vinaweza kusababisha mabadiliko ya hali, hususan kabla ya kipindi cha hedhi au baada ya kupata mtoto

  • Umepitia tukio la kihisia, kama vile jana la kiasili (kwa mfano tufani), ugonjwa mbaya, au kifo cha mwanafamilia

  • Una matatizo makubwa ya afya, kama vile kansa

  • Unatumia dawa ambazo mojawapo ya athari zake ni mfadhaiko

Mfadhaiko hutokea sana wakati kuna mwangaza mdogo sana wa mchana, kama vile msimu wa mapukutiko na msimu wa baridi.

Je, dalili za mfadhaiko ni zipi?

Dalili zinaweza kuanza polepole

  • Kupungua kwa hamu ya kushiriki katika shughuli ulizokuwa ukizipenda zamani

  • Kujihisi kuwa hufai, majisuto au upweke

  • Kuhisi kuwa huna matumaini

  • Mabadiliko kwenye tabia za kulala, kama vile kulala zaidi, kutatizika kupata usingizi, au kuamka asubuhi sana

  • Kupungua au kuongeza uzani

  • Kuwa na changamoto katika kumakinika na kufanya maamuzi

  • Kunywa pombe, kuvuta sigara au kutumia dawa za kulevya mara nyingi kuliko kawaida

  • Kufikiria kuhusu kifo na kujiua

Madaktari wanajuaje kujua iwapo nini mfadhaiko?

Madaktari watakisia kuwa una mfadhaiko kulingana na dalili zako na historia ya familia ya mfadhaiko. Pia watakuuliza maswali ili kubaini kiwango cha mfadhaiko wako. Ili kubaini iwapo tatizo la afya linasababisha mfadhaiko wako, madaktari wanaweza kufanya vipimo, kama vile vipimo vya damu.

Madaktari hutibu vipi tatizo la mfadhaiko?

Huenda daktari:

  • Kupendekezea dawa za kuzuia msongo wa mawazo

  • Kutoa usaidizi wa ushauri nasaha wa kibinafsi au vikundi (matibabu ya kisaikolojia)

  • Kukushauri upate matembezi kidogo na utembelee marafiki na familia

  • Kukualika kwenye kikundi cha usaidizi ili usimulie hisia zako kwa wengine

  • Kukulaza hospitalini ikiwa unafikiria kuhusu kujiua au ukijaribu kitendo hicho

Ikiwa una mfadhaiko mbaya sana, madaktari wanaweza kufanya tiba ya mshtuko wa umeme (ambayo awali iliitwa tiba ya kushtua ubongo). Katika tiba ya mshtuko wa umeme, daktari wako atakupa dawa ili ulale kisha atapitisha umeme kwenye ubongo wako. Madaktari hawajui kwa nini, lakini umeme mara nyingi husaidia kuondoka mfadhaiko.

Ikiwa mfadhaiko wako hutokea msimu wa mapukutiko au msimu wa baridi, madaktari wanaweza kukuelekeza uangalie taa angavu zinazoiga mwangaza wa jua (tiba ya nuru).