Ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi (RA)

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2024

Ugonjwa wa baridi yabisi ni magonjwa ambayo husababisha viungo kupata maumivu, kuvimba na kuwa vyekundu. Kuna aina nyingi za ugonjwa wa baridi yabisi.

Ni nini maana ya ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi (RA)?

RA ni aina ya ugonjwa wa baridi yabisi ambapo mfumo wa kingamaradhi wa mwili wako hushambulia viungo vyako.

  • RA hutokea sana kwa wanawake na kwa kawaida huanza kwa watu walio na umri wa kati ya miaka 35 na 50, lakini inaweza kuanza mapema

  • Inaweza kuathiri kiungo chcochote lakini inatokea sana kwenye mikono na miguu

  • Viungo huwa vimefura, kukakamaa na kusababisha maumivu asubuhi na mara nyingi huharibika umbo baada ya miaka mingi

  • Wakati mwingine RA huathiri sehemu zingine za mwili wako, ikiwa ni pamoja na moyo, mapafu, macho na mishipa ya damu

  • Madaktari wanaweza kujua iwapo una RA kulingana na dalili zako, eksirei na vipimo vya damu

  • Matibabu yanaweza kujumuisha dawa, mazoezi na wakati mwingine upasuaji

Je, nini husababisha ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi?

RA ni ugonjwa wa mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili. Mfumo wa kingamwili ni sehemu ya mfumo wa ulinzi mwilini mwako, ambao hukukinga dhidi ya ugonjwa na maambukizi. Katika ugonjwa wa mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili, mfumo wako wa kingamwili hushambulia sehemu za mwili wako mwenyewe kwa bahati mbaya—katika RA, mfumo wako wa kingamaradhi hushambulia viungo vyako na wakati mwingine sehemu zingine za mwili wako. Madaktari hawajui ni nini haswa husababisha mfumo wa kingamaradhi ushambulie viungo vyako.

Dalili za ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi ni zipi?

Dalili kwa kawaida huanza taratibu.

Dalili zilizozoeleka zaidi zinajumuisha:

  • Viungo vyekundu, vyenye joto, vilivyofura na vinavyosababisha maumivu vinapoguswa (uvimbe), kwa kawaida huwa viungo sawa vya pande zote mbili za mwili wako (kama vile vifundo vyote viwili vya mikono au magoti yote mawili)

  • Kukakamaa kwa viungo vilivyoathiriwa kwa takribani saa moja baada ya kuamka asubuhi

Pamoja na maumivu ya viungo, huenda ukajihisi mgonjwa na kuonyesha dalili kama vile:

  • Homa kiasi

  • Kuhisi uchovu mwingi

  • Kukosa hamu ya kula na kupoteza uzani

Baada ya muda, iwapo tatizo la viungo litazidi, huenda:

  • Ukashindwa kuinama au kufungua viungo kikamilifu

  • Ukapata uharibifu wa kudumu wa umbo la viungo, hususan kwenye mikono na vidole vyako

When the Fingers Are Abnormally Bent

Some disorders, such as rheumatoid arthritis, and injuries can cause the fingers to bend abnormally. In swan-neck deformity, the joint at the base of the finger bends in (flexes), the middle joint straightens out (extends), and the outermost joint bends in (flexes). In boutonnière deformity, the middle finger joint is bent inward (toward the palm), and the outermost finger joint is bent outward (away from the palm).

Unaweza pia kupata matatizo yasiyohusiana na viungo vyako. Kwa mfano, huenda:

  • Macho mekundu, yanayowasha

  • Matatizo ya moyo au mapafu yanayosababisha maumivu ya kifua au shida ya kupumua

  • Uvimbe mgumu kwenye ngozi ya mikono au miguu

Watu wengi walio na RA hupata ulemavu wa aina fulani lakini bado wanaweza kuendelea na maisha ya kawaida. Baadhi ya watu huwa walemavu kabisa, kama wale walio na madhara makubwa ya umbo la viungo vya mikono.

Daktari wangu atajua vipi kuwa nina ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi?

Daktari wako anaweza kujua iwapo una RA kutokana na:

  • Dalili zako

  • Vipimo vya damu

  • Eksirei

  • Kupima majimaji ya kiungo

Madaktari hutibu vipi ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi?

Madaktari hutibu RA kwa dawa zinazoweza:

  • Kupunguza kuvimba na kudhibiti dalili

  • Kupunguza maendeleo ya RA na kuzuia viungo visiharibike umbo

  • Kupunguza nguvu za mfumo wa kingamaradhi ili kupunguza dalili

Madaktari wanaweza kupendekeza:

  • Upate mapumziko ya mara kwa mara

  • Ule milo yenye kiwango kikubwa cha samaki na mafuta yaliyotokana na mimea lakini isiwe na kiwango kikubwa cha nyama nyekundu

  • Ufanye mazoezi (zungumza na daktari wako kuhusu mazoezi yanayokufaa)

  • Usivute sigara

Huenda madaktari pia wakapendekeza: