Hashimoto thairoditisi

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Dundumio yako inapatikana chini ya kongomeo kwenye shingo yako.

Dundumio lako hutengeneza homoni za dundumio. Homoni hudhibiti kasi ya utendakazi wa kemikali za mwili wako (kiwango cha kimetaboli). Karibu kila seli mwilini inahitaji homoni za dundumio. Miongoni mwa majukumu mengine mengi, homoni za dundumio husaidia kudhibiti:

  • Jinsi mwili unavyotumia kalori

  • Jinsi moyo wako unavyopiga haraka

  • Joto la mwili wako

Locating the Thyroid Gland

Hashimoto thairoditisi ni nini?

Ukiwa na ugonjwa wa Hashimoto thairoditisi, mfumo wa kingamaradhi wa mwili wako unashambulia kimakosa dundumio lako. Aina hii ya ugonjwa huitwa ugonjwa wa mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili.

  • Tezi dundumio yako inakuwa kubwa na inaacha kutengeneza homoni za kutosha (dudumio lisilokuwaamilifu)

  • Watu wenye dundumio lisiloamilifu kwa kawaida wanahisi kuchoka na wanapata mafua kwa urahisi

  • Ikiwa utapata dundumio lisiloamilifu, utahitaji kutumia vidonge vya homoni ya dudumio kwa maisha yako yote

Nini kinasababisha Hashimoto thairoditisi?

Madaktari hawajui kwa nini mfumo wa kingamaradhi wa mwili wako unashambulia kimakosa tezi dundumio yako. Unapatikana sana kwa wanawake wenye umri wa kati una kawaida ya kukaa kwenye familia. Wakati mwingine huwapata watu wenye matatizo mengine ya mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi

Dalili za Hashimoto thairoditisi ni zipi?

Mapema, huenda usione dalili au unaweza kugundua:

  • Tezi dudumio iliyovimba kidogo, ngumu isiyo na maumivu

  • Kuhisi umevimba shingo

Ikiwa dudumio lako litaacha kutengeneza homoni za kutosha, utapata dalili za dundumio lisiloamilifu, kama vile:

  • Kuhisi kuchoka

  • Kuhisi baridi haraka

  • Macho na uso uliovimba, kope zilizoinama

  • Nywele nyembamba, kavu

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina Hashimoto thairoditisi?

Madaktari watafanya:

Je, madaktari wanatibu vipi Hashimoto thairoditisi?

Hakuna matibabu ya Hashimoto thairoditisi yenyewe.

Ikiwa una dudumio lisiloamilifu, madaktari watakupa:

  • Vidonge vya homoni za dundumio

Mara baada ya matibabu kuanza, madaktari wataanza kurekebisha taratibu dozi ya vidonge vya homoni kulingana na vipimo vya damu.