Matatizo ya kiafya yanayoathiri ubongo wako mara nyingi hukuzuia kuwa macho na kufikiri vizuri. Unaweza kuathirika kidogo tu au sana, kuanzia kuwa:
Kupoteza kidogo utayari kuliko kawaida
Kuchanganyikiwa na kushindwa kueleweka
Kuwa mweye usingizi na ngumu kuamshwa
Kupoteza fahamu
Mzubao ni nini?
Mzubao ni pale unapoonekana una usingizi au usingizi mzito, ikiwa kama umezimia Unaamka kidogo watu wakikupigia kelele au kukutingisha au kukufinya. Lakini baada ya kuacha kufanya hivyo, unarudia tena kusinzia.
Haichukuliwi kuwa ni mzubao ikiwa umechoka tu na unahisi usingizi kutokana na kutolala kwa muda mrefu.
Je, usingizi mzito ni nini?
Usingizi mzito ni pale unapopoteza ufahamu na huwezi kuamshwa, haijalishi watu watajaribu mara ngapi.
Je, nini husababisha mzubao au usingizi mzito?
Sababu za mzubao au usingizi mzito zinafanana sana, na ni pamoja na:
Matatizo ya mwili mzima kama vile:
Sumu, kama vile monoksidi kaboni
Pombe na dawa za kulevya kama vile opioids
Viwango vya chini vya sukari kwenye damu au viwango vya juu vya sukari kwenye damu
Ini kushindwa kufanya kazi
Figo kushindwa kufanya kazi
Matatizo ya ubongo kama vile:
Jeraha la kichwa
Maambukizi makali ya ubongo, kama vile homa ya uti wa mgongo
Mtiririko mdogo wa damu kwenda kwenye ubongo kama inavyoweza kutokea kwa kiharusi
Dalili za mzubao na usingizi mzito ni zipi?
Kwa mzubao, dalili kuu ni:
Kuonekana uko usingizini na kuwa vigumu sana kukuamsha
Ukiwa macha, kutokujibu maswali au kutoeleweka
Kurudi usingizini usipochangamshwa
Kwa usingizi mzito, watu hupoteza fahamu na:
Hawaamshwi na msisimko wowote
Wakati mwingine upumuaji wao sio wa kawaida (kama vile usio wa kawaida au kwa haraka au taratibu sana)
Wakati mwingine wana kasoro kwenye macho yao, kama vile mboni kubwa au ndogo, macho ambayo hayasongi, au macho yanayosonga kwa njia za ajabu
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtu anakabiliwa na mzubao au usingizi mzito?
Madaktari wanaweza kufahamu kama mtu anakabiliwa na mzubao au usingizi mzito kwa kumchunguza mtu huyo.
Ili kugundua chanzo cha mzubao au usingizi mzito, madaktari hufanya vipimo, kama vile:
Vipimo vya damu
Vipimo vya mkojo
Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) au MRI (picha inayoonyesha sehemu ya ndani ya mwili wako) ya kichwa
Elektroensefalografia (EEG—kipimo kisicho umiza ambacho hurekodi shughuli za umeme za ubongo)
Je, madaktari hutibu vipi mzubao na usingizi mzito?
Watu wanahitaji kuwa hospitalini, kwa kawaida kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) Mara nyingi wanahitaji:
Vifuatiliaji vya mapigo ya moyo na shinikizo la damu
Bomba la oksijeni au kupumua
Majimaji au dawa zinazoingizwa moja kwa moja kwenye mishipa (IV)
Madaktari watatibu chanzo cha mzubao au usingizi mzito. Matibabu yanaweza kujumuisha:
Viuasumu vya dawa au sumu
Dawa za kuua bakteria kwa ajli ya maambukizi
Upasuaji wa ubongo kwa ajili ya mkusanyiko wa damu au majimaji yaliyozunguka ubongo
Wagonjwa ambao huendelea kuwa kwenye usingizi mzito wanahitaji huduma za usaidizi, kama vile:
Mpira wa chakula kwa ajli ya maji na chakula
Kugeuza kila mara mwili wa huyo mtu ili kuzuia vidonda vitokanavyo na kulala kwa muda mrefu na damu kuganda
Kusogeza mikono na miguu ya huyo mtu kila mara ili kuzuia misuli kukaza (kukakamaa)
Mrija (katheta) kwenye kibofu cha mkojo ili kutoa mkojo
Matone ya macho ili kuepusha macho ya mtu huyo kukauka
Hali ya mtu hutegemea sababu iliyosababisha usingizi mzito. Baadhi ya matatizo hupotea, na mtu hupona kabisa. Watu wengine huamka lakini huwa na uharibifu fulani kwa ubongo na hawarudi kuwa kawaida. Watu wenye uharibifu mkubwa wa ubongo wanaweza kubaki kwenye usingizi mzito. Wachache hupata hali ya kuwa macho pasipo ufahamu.