Hali ya kuwa macho pasipo ufahamu

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2024

Je, hali ya kuwa macho pasipo ufahamu ni nini?

Hali ya kuwa macho pasipo ufahamu ni pale watu walio na uharibifu wa ubongo wanaonekana kuwa macho lakini hawafanyi vitendo vyovyote vya kukusudia au kuitikia kile kinachoendelea karibu yao.

  • Mtu aliye na hali ya kuwa macho pasipo ufahamu hufanya vitendo vya msingi vinavyotokea kiotomatiki, kama vile kupumua, kukohoa, kupiga miayo, au kumeza lakini hafanyi chochote kwa kukusudia.

  • Baadhi ya watu hupona, lakini wengi wao wanakufa ndani ya miezi 6

  • Watu ambao wako katika hali ya kuwa macho pasipo ufahamu kwa muda mrefu zaidi ya miezi michache hawana uwezekano wa kupona

Hali ya kuwa macho pasipo ufahamu ni tofauti na usingizi mzito kwa kuwa macho ya watu yamefunguliwa na wanaonekana kuwa macho.

Je, nini husababisha hali ya kuwa macho pasipo ufahamu?

Hali ya kuwa macho pasipo ufahamu hutokea pale:

  • Sehemu ya ubongo ambayo hudhibiti kutafakari na utambuzi inapoacha kufanya kazi

  • Sehemu ya ubongo inayodhibiti kupumua, mapigo ya moyo na shinikizo la damu huendelea kufanya kazi

Chanzo hujumuisha uharibifu mkubwa wa udongo unaotokana na:

Dalili za hali ya kuwa macho pasipo ufahamu ni zipi?

Watu wenye hali ya kuwa macho pasipo ufahamu wanaweza:

  • Kufungua macho na kupepesa

  • Kulala na kuamka kwa kufuata ratiba ya kawaida

  • Kufanya matendo ya msingi kiotomatiki, kama vile kupumua, kunyonya, kutafuna, kugooka, na kumeza

  • Kushtushwa na sauti kubwa

Watu wenye hali ya kuwa macho pasipo ufahamu hawawezi:

  • Kutambua mambo yanayoendelea katika mazingira yaliyowazunguka

  • Kuzungumza au kufuata maelekezo

  • Kufikiri au kusogeza miili yao kwa makusudi, kama vile kujiondoa kwenye kitu kinachowaumiza

  • Kudhibiti mkojo au kinyesi

Watu wenye ufahamu kidogo wanaweza kuwa katika hali ya utambuzi kidogo.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtu ana hali ya kuwa macho pasipo ufahamu?

Madaktari hushuku uwepo wa hali ya kuwa macho pasipo ufahamu kulingana na dalili za mtu husika. Ili kuthibitisha, huenda daktari akafanya yafuatayo:

  • Humchunguza mtu kwa karibu kwa kipindi fulani ili kuona kama mtu huyo ana utambuzi na kuitikia

  • Hufanya vipomo, kama vile MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) au uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) wa kichwa

  • Hufanya Elektroensefalografia (EEG—kipimo kisicho umiza ambacho hurekodi shughuli za umeme za ubongo)

Je, madaktari hutibu vipi hali ya kuwa macho pasipo ufahamu?

Hakuna matibabu ya kuboresha hali ya kuwa macho pasipo ufahamu. Wakati mwingine, watu hupata ahueni wao wenyewe kutegemea na lipi lilikuwa tatizo lao la mwanzo na kiwango cha ukubwa wa tatizo hilo. Watu hawarudi kuwa kawaida, lakini wachache hujifunza tena jinsi ya kuzungumza na kuwaelewa watu.

Mtu mwemye hali ya kuwa macho pasipo ufahamu anahitaji uangalizi wa muda mrefu, pamoja na:

  • Mpira wa chakula

  • Kugeuza kila mara mwili wa mtu huyo ili kuzuia vidonda vitokanavyo na kulala kwa muda mrefu

  • Dawa ya kuzuia damu kuganda

  • Kusogeza mikono na miguu ili kuzuia misuli kukaza

  • Mrija (katheta) kwenye kibofu cha mkojo ili kutoa mkojo

  • Kumsafisha na kumwogesha

Ikiwa mtu amekuwa katika hali ya kuwa macho pasipo ufahamu kwa muda mrefu na haonyeshi dalili zozote za kupona, madaktari watazungumza na familia kuhusu kutompatia matibabu ya kumfanya aendelee kuishi iwapo atapata ugonjwa mpya au wa ziada. Madaktari na familia ya mtu huyo watazingatia kile ambacho huyo mtu angependa na kupitia maelekezo yoyote yaliyo kwenye wosia wa maisha (mwongozo wa mapema).