Homa ya uti wa mgongo iliyosababishwa na bakteria

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2024

Homa ya uti wa mgongo iliyosababishwa na bakteria ni nini?

Homa ya uti wa mgongo ni maambukizi ya tishu nyembamba inayofunika ubongo na uti wa mgongo wako. Safu hii ya tishu inajulikana kama utando. Katika homa ya uti wa mgongo ya bakteria, maambukizi kwenye uti wa mgongo husababishwa na bakteria. Bila matibabu, homa ya uti wa mgongo inaweza kuharibu ubongo wako na kusababisha kifo. Kwa sababu hiyo, homa ya uti wa mgongo kutokana na bakteria ni dharura. Homa ya uti wa mgongo iliyosababishwa na virusi (homa ya uti wa mgongo kutokana na virusi) si hatari sana.

  • Watoto wakubwa na watu wazima walio na homa ya uti wa mgongo hupata homa, maumivu ya kichwa na shingo iliyokaza

  • Watoto walio na umri wa chini ya miaka 2 hupata homa na kuonekana kuwa na usumbufu lakini hawapati shingo iliyokaza

  • Kadiri ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo unavyozidi, watu hupatwa na usingizi na kuchanganyikiwa kisha wanazimia kwa muda mrefu

  • Ili kutambua ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo, madaktari hufanya utaratibu wa kufyonza majimaji ya uti wa mgongo

  • Madaktari hutumia dawa za kuua bakteria kutibu homa ya uti wa mgongo iliyosababishwa na bakteria, haraka iwezekanavyo

  • Chanjo zinaweza kuzuia baadhi ya aina za homa ya uti wa mgongo

Homa ya uti wa mgongo iliyosababishwa na bakteria ni hatari na inaweza kuleta matatizo makubwa isipotibiwa. Ikiwa unafikiri kuwa wewe au mtu mwingine ana homa ya uti wa mgongo, nenda hospitalini mara moja.

Tishu Zinazofunika Ubongo

Kwenye fuvu la kichwa, ubongo umefunikwa na safu 3 za tishu zinazoitwa tando.

Ni kitu gani husababisha homa ya uti wa mgongo inayotokana na bakteria?

Homa ya uti wa mgongo iliyosababishwa na bakteria hutokea pale ambapo bakteria inaingia kwenye majimaji yaliyo katikati ya ubongo wako na utando mwembamba wa tishu unaofunika ubongo wako. Huenda ukapata bakteria hiyo kutoka kwa:

Aina tofauti za bakteria zinaweza kusababisha homa ya uti wa mgongo Aina ya bakteria iliyokuathiri hutegemea umri wako, uwezo wa mfumo wako wa kingamwili, na jinsi ulivyopata maambukizi.

Ni mambo gani huongeza hatari ya kuugua homa ya uti wa mgongo kutokana na bakteria?

Homa ya uti wa mgongo iliyosababishwa na bakteria haitokei mara nyingi lakini una uwezekano mkubwa wa kuugua ugonjwa huo iwapo:

  • Ulikaribiana na mtu anayeugua homa ya uti wa mgongo

  • Hujapata sindano (chanjo) zako zote

Pia, uko katika hatari kubwa iwapo:

  • Una mfumo dhaifu wa kingamwili

  • Ulifanyiwa upasuaji kwenye ubongo au uti wa mgongo hivi majuzi

  • Una kasoro ya kuzaliwa kwenye fuvu la kichwa au uti wa mgongo

Je, ni zipi dalili za homa ya uti wa mgongo iliyosababishwa na bakteria?

Dalili ni tofauti kulingana na umri wa mtu. Katika umri wowote, dalili zinaweza kukithiri. Kwa hivyo iwapo unafikiria kuwa mtu ana dalili za homa ya uti wa mgongo, mpeleke kwa daktari mara moja.

Dalili za homa ya uti wa mgongo kwa watoto wachanga na watoto wengine

Mwanzoni, watoto wanaweza kuwa na homa tu bila kuonekana kana kwamba ni wagonjwa sana. Hata hivyo, watoto wanaweza kupata dalili zingine kwa haraka, kama vile:

  • Upele

  • Kukataa kula

  • Kuwa na usumbufu au usingizi kwa njia isiyo ya kawaida

  • Vifafa

Kinyume na watoto wakubwa, watoto walio na umri wa chini ya miaka 2 huwa hawapati shingo iliyokaza.

Dalili za homa ya uti wa mgongo kwa watoto wakubwa na watu wazima

Watoto wakubwa na watu wazima huanza kwa dalili zisizokithiri zinazofanana na za mafua au maambukizi mengine ya virusi. Punde baadaye wanapata:

  • Homa

  • Maumivu ya kichwa yasiyopungua

  • Shingo iliyokaza

  • Wakati mwingine upele wa madoa au alama za zambarau

Kadiri homa ya uti wa mgongo inavyozidi, watoto wakubwa na watu wazima wanaweza:

  • Kuchanganyikiwa au kupoteza umakinifu

  • Kupata vifafa

  • Kupoteza fahamu kwa muda mrefu

Je, ni yapi matatizo yanayoweza kutokana na homa ya uti wa mgongo?

Watoto waliougua homa ya uti wa mgongo wakati mwingine hupata matatizo ya kudumu ya ubongo na neva kama vile:

Madaktari wanaweza kujuaje kuwa ninaugua homa ya uti wa mgongo?

Madaktari hufanya vipimo vya kutafuta bakteria kwenye majimaji yanayozunguka ubongo na uti wako wa mgongo (majimaji ya uti wa mgongo). Ili kupata umajimaji wa uti wa mgongo, madaktari:

Wakati wa kukinga majimaji ya uti wa mgongo, madaktari hudunga sindano ndefu, nyembamba kwenye sehemu ya chini ya mgongo wako. Wanavuta majimaji kidogo ya uti wa mgongo kwa ajili ya vipimo. Kabla ya kutekeleza ukingaji wa majimaji ya uti wa mgongo, madaktari wakati mwingine hufanya MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) au uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta).

Jinsi ya Kufanya Kinga Majimaji ya Uti wa Mgongo

Majimaji ya uti wa mgongo hutiririka kupitia mkondo katikati ya safu ya kati na ya ndani ya tishu (tando) zinazofunika ubongo na uti wa mgongo. Ili kutoa sampuli ya majimaji haya, daktari huingiza sindano ndogo, yenye mrija katikati ya mifupa miwili (vifupa vya uti wa mgongo) kwenye sehemu ya chini ya uti wa mgongo, chini ya mahali ambapo uti wa mgongo huishia. Kwa kawaida, anayefanyiwa vipimo hulalia upande na kukunja magoti kukaribia kifua. Mkao huu huongeza nafasi kati ya vifupa vya uti wa mgongo, ili daktari asiguse mifupa anapoingiza sindano.

Madaktari hukusanya majimaji ya uti wa mgongo kwenye mirija ya vipimo na kuyapeleka kwenye maabara kwa vipimo.

Madaktari hutibu vipi homa ya uti wa mgongo?

Madaktari wakishuku kuwa una homa ya uti wa mgongo, watakupatia:

  • Dawa moja au zaidi za kuua bakteria kupitia mshipa (IV)

Kwa kuwa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo unaotokana na bakteria unaweza kukithiri kwa haraka sana, watakupa dawa za kuua bakteria haraka iwezekanavyo, wakati mwingine hata kabla hawajamaliza kufanya vipimo. Kwa kuwa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo unaotokana na bakteria unaweza kusababisha matatizo makubwa, utahitaji kukaa hospitalini, pengine kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Pamoja na dawa za kuua bakteria, madaktari wanaweza kukupatia kotikosteroidi. Kotikosteroidi zinaweza kusaidia kuzuia matatizo kwa kupunguza kufura na kuvimba kwenye ubongo na neva zako.

Watu wengi hupona kabisa kutokana na homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na bakteria ikiwa watapata matibabu mara moja. Kusubiri sana kabla ya kupata matibabu kunaweza kuwa hatari au hata kusababisha kifo.

Je, ninawezaje kuzuia kuugua homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na bakteria?

Mikakati miwili muhimu ni:

  • Chanjo

  • Dawa za kuua bakteria

Chanjo zinapatikana ili kuzuia baadhi ya aina za homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na bakteria Baadhi ya chanjo zinapendekezwa kwa kila mtu na zimejumuishwa kwenye sindano za kawaida za utotoni. Chanjo nyinginezo ni za watu walio katika hatari kubwa pekee:

  • Watoto walio na umri wa kati ya miaka 2 na 10 walio na mfumo dhaifu wa kingamwili

  • Wanafunzi wanaoishi kwenye mabweni

  • Makuruta wa jeshi

  • Watu wanaosafiri kwenda maeneo ambako homa ya uti wa mgongo inapatikana sana

  • Watu ambao kazi zao zinawaweka hatarini, kama vile wafanyakazi katika maabara ya kimatibabu

Muulize daktari wako kuhusu chanjo ambazo wewe na watoto wako mnapaswa kupata.

Ikiwa umekaribiana na mtu anayeugua homa ya uti wa mgongo, madaktari watakupatia dawa za kuua bakteria ili kupuunguza uwezekano wako wa kuugua ugonjwa huo.