Nyenzo za Mada
Haidrosefalasi ni nini?
Haidrosefalasi ni hali ya kuwepo kwa kiasi kikubwa cha maji ndani ya kichwa. Wakati mwingine hujulikana kama "maji kwenye ubongo."
Ubongo wako una nafasi kadhaa zilizo wazi ambazo ndani yake zimejaa majimaji. Kwenye haidrosefalasi, nafasi hizi huwa na majimaji mengi.
Majimaji ya ziada kwenye ubongo yanaweza kufanya kichwa cha mtoto wako kiongezeke ukubwa
Ikiwa shinikizo litaongezeka sana kwenye ubongo, mtoto anaweza kupata matatizo
Majimaji yanaweza kujikusanya kwa sababu ya kasoro ya kuzaliwa, kuvuja damu ndani ya ubongo, au uvimbe wa ubongo
Madaktari hufanya utaratibu wa kutoa hayo majimaji ya ziada
Je, nini husababisha haidrosefalasi?
Fuvu la mtoto limeundwa na mifupa mbalimbali. Kwa miaka michache ya mwanzo, mifupa hii huwa imeunganishwa pasipo kukaza. Baadaye, mifupa hukua kwa pamoja na kuwa mfupa mmoja imara. Lakini kabla ya mifupa kukua kwa pamoja, kuongezeka kwa shinikizo la majimaji katika ubongo kunaweza kufanya mifupa itengane. Hii huzuia shinikizo kuongezeka sana, lakini hufanya kichwa cha mtoto kuongezeka ukubwa zaidi. Mafuvu ya watoto wakubwa na watu wazima hayawezi kupanuka, hivyo kuongezeka kwa shinikizo huharibu ubongo na hali hii inaweza kuwa mbaya kwa haraka sana.
Mambo yafuatayo yanaweza kusababisha majimaji ya ziada kwenye ubongo:
Hitilafu kwenye ubongo wakati wa kuzaliwa
Kuvuja damu ndani ya ubongo
Uvimbe kwenye ubongo
Maambukizi ya ubongo
Watoto wanaweza kuzaliwa wakiwa na haidrosefalasi, au inaweza kuwapata baada ya kuzaliwa.
Dalili za haidrosefalasi ni zipi?
Dalili za haidrosefalasi zinategemea sehemu na kiasi cha majimaji yaliyopo. Mtoto mchanga mwenye haidrosefalasi anaweza:
Kuwa na kichwa kikubwa kisicho cha kawaida
Kuwa na mahangaiko au kutovutiwa na kitu chochote
Kuanza kulia kwa sauti ya juu
Kutapika kwa nguvu
Kupata vifafa
Kuwa na uvimbe kwenye sehemu laini za fuvu
Kuwa na jicho moja linalotazama upande tofauti na jicho jingine (macho yanayopisha)
Watoto wakubwa wanaweza kupata maumivu ya kichwa, kuwa na matatizo ya kuona, au vyote.
Ikiwa haitatibiwa, watoto wenye haidrosefalasi wanaweza kuwa na udhaifu wa kujifunza au kupoteza uwezo wa kuona.
STEVE ALLEN/MAKTABA YA PICHA ZA SAYANSI
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana haidrosefalasi?
Madaktari hufanya vipimo vya kila mara kabla na baada ya mtoto kuzaliwa ili kupima uwepo wa haidrosefalasi:
Kabla ya kuzaliwa, madaktari watafanya kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti na kupima ukubwa wa kichwa cha mtoto
Baada ya mtoto kuzaliwa, madaktari watapima ukubwa wa kichwa kwa kutumia utepe wa kupimia na ikiwa ni kikubwa, wanaweza kufanya Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) au MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku), au kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa kichwa
Je, madaktari hutibu vipi haidrosefalasi?
Madaktari hutibu haidrosefalasi kwa kutumia njia mbalimbali kwa kutegemea chanzo chake, kiasi cha majimaji yaliyopo, na ikiwa hali yake inazidi kubwa mbaya.
Ikiwa hakuna majimaji mengi ya ziada na hali yake haizidi kuwa mbaya, mtoto wako anaweza asihitaji kupatiwa matibabu.
Ili kusaidia kupunguza dalili kwa muda mfupi, madaktari wanaweza:
Kuondoa majimaji kwa kutumia sindano iliyopenyezwa kwenye ubongo au wakati mwingine kwenye sehemu ya chini ya mgongo (kufyonza majimaji ya uti wa mgongo)
Ikiwa kuna majimaji mengi au majimaji yanasababisha uwepo wa dalili, madaktari wanaweza:
Kuingiza bomba jembamba la plastiki linaloitwa shanti ili kutoa majimaji kwenye ubongo
Kufanya upasuaji wa ubongo ili kurekebisha tatizo ambalo linasababisha majimaji kujikusanya
Kwa uwepo wa shanti, upande mmoja wa bomba la plastiki huwa kwenye eneo lililojaa majimaji kwenye ubongo. Bomba huwekwa chini ya ngozi ya mtoto na upande mwingine huingia ndani ya tumbo. Hii hutengeneza njia ya majimaji kutoka kwenye ubongo.
Mara nyingi shanti huwa ni za kudumu, lakini muda mwingine madaktari wanaweza kuziondoa pale mtoto anapokua.
Shanti inaweza kuziba, kuvunjika au kupata maambukizi. Hili likitokea, shanti inaweza kubadilishwa.