Mgongo Wazi

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2022 | Imebadilishwa Jul 2023

Mgongo wazi ni nini?

Mgongo wazi ni kasoro ya mgongo ya kuzaliwa nayo. Mgongo wa mtoto ambaye hajazaliwa haumbwi kama kawaida. Mara nyingine uti wa mgongo na neva zinazotoka ndani yake huathiriwa. Hili linaweza lisisababishe tatizo, au linaweza kusababisha matatizo ya muda mrefu ya kutembea, kukojoa au kujisadia.

  • Mgongo wazi huathiri sehemu ya kati na chini ya mgongo

  • Watoto wachache pia hupata kasoro kwenye ubongo

  • Kasoro hizi zinaweza kuwa ndogo hadi kubwa

  • Kwa kawaida kasoro ndogo hazina dalili

  • Kasoro kubwa zinaweza kusababisha udhaifu kwenye miguu na matatizo ya kutembea, mgongo kupinda, au matatizo ya kibofu cha mkojo

  • Uharifu wa ubongo au uti wa mgongo una uwezekano mkubwa wa kutokea ikiwa tishu zitavimba na kutokeza kwa mgongo wa mtoto

  • Ikiwa sehemu za uti wa mgongo zitatoka nje, mtoto anaweza kupata maambukizi (homa ya uti wa mgongo)

Mgongo Wazi: Kasoro ya Mgongo

Katika mgongo wazi, mifupa ya mgongo (pingili za uti wa mgongo) haiumbwi kama kawaida. Ukubwa wa tatizo la mgongo wazi unaweza kutofautiana.

Katika hali ya kufichwa matatizo ya uti wa mgongo ya kuzaliwa nayo, pingili moja au mbili haziumbwi kama inavyotakiwa, na uti wa mgongo na matabaka ya tishu (meningi) zinazouzunguka nazo pia zinaweza kuathiriwa. Kuna aina kadhaa zilizo na ukali tofauti wa kinyulojia. Utambuzi wa ugonjwa huu wakati mwingine hutokana na dalili zake katika eneo la chini la mgongo, kama vile kishungi cha nywele, kubonyea, au eneo lenye rangi ya asili kwenye ngozi iliyo juu ya eneo lenye kasoro.

Kwa meningoseli, meninges huchomoza kupitia pingili ambazo uumbaji wake haukukamilika, hivyo kusababisha uvimbe uliojaa majimaji chini ya ngozi. Uti wa mgongo uko katika mahali pake pa kawaida.

Aina mbaya zaidi ni meningomayeloseli, ambapo meninges na pingili huchomoza. Eneo lililoathiriwa huonekana ni bichi na lenye rangi nyekundu, na mtoto mchanga ana uwezekano mkubwa wa kudhoofika.

Je, nini husababisha tatizo la mgongo wazi?

Sababu za mgongo wazi ni pamoja na:

  • Kutokuwa na vitamini ya kutosha ya asidi ya foliki kabla na wakati wa ujauzito

  • kasoro ya kijenetiki

  • Matumizi ya aina fulani ya dawa wakati wa ujauzito, kama vile valproate

Dalili za mgongo wazi ni zipi?

Watoto wengi wenye kasoro ndogo huwa hawana dalili. Dalili nyingi hutokana na uharibifu wa ubongo au uharibifu wa uti wa mgongo. 

Dalili zinajumuisha:

  • Majimaji mengi kwenye uwazi wa ndani ya ubongo (haidrosefalas)

  • Shida ya kujifunza

  • Ugumu wa kumeza

  • Ugumu wa kutembea

  • Upungufu wa hisia za kawaida katika ngozi iliyo juu ya uti wa mgongo

  • Kushindwa au ugumu wa kukojoa

  • Maambukizi ya kila mara ya njia ya mkojo

  • Kushindwa kudhibiti kinyesi kutoka

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto ana mgongo wazi?

Madaktari hufanya uchunguzi wakati wa kipindi cha 2 cha miezi mitatu ya ujauzito. Hii hujumuisha:

Je, madaktari hutibu vipi tatizo la mgongo wazi?

Kwa kawaida, madaktari hufanya upasuaji.

  • Timu ya wataalamu wataamua juu ya aina na kiwango cha ukali wa tatizo, na kisha kuzungumza na familia kuhusu matibabu na matunzo

  • Madaktari watatibu tatizo la kibofu cha mkojo, mfupa, msuli, na sehemu nyingine

Je, tatizo la mgongo wazi linaweza kuzuiwa?

Madaktari hupendekeza wanawake wote ambao wanaweza kupata ujauzito au ambao ni wajawazito kutumia vitamini ya asidi ya foliki (folati). Tafiti zinaonyesha kuwa asidi ya foliki husaidia kukinga dhidi ya mgongo wazi na kasoro sawa na hizo kwa watoto ambao hawajazaliwa.

  • Mwanamke ambaye amepata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi ana uwezekano mkubwa wa kupata mtoto mwingine mweye kasoro sawa na hiyo, na anatakiwa kutumia dozi kubwa ya vitamini za asidi ya foliki kuanzia miezi 3 kabla ya kubeba ujauzito na aendelee kutumia kwa kipindi chote cha 1 cha miezi mitatu ya ujauzito

Zungumza na daktari wako kuhusu kiasi cha asidi ya foliki unachotakiwa kutumia.