Kichwa Kidogo cha Mtoto

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2024

Kichwa kidogo ni nini?

Hali ya kichwa kidogo ni kichwa kidogo kisicho cha kawaida.

  • Kwa kawaida mtoto mwenye kichwa kidogo anakuwa na ubongo mdogo, na ubongo unaweza usiwe umeundwa vizuri

  • Hali ya kichwa kidogo ni nadra kutokea

  • Hali ya kichwa kidogo inaweza kusababishwa na matatizo mengi ambayo hutokea kwenye mfuko wa uzazi, ikijumuisha maambukizi, ukosefu wa oksijeni, ukosefu wa lishe nzuri, na kasoro za kuzaliwa za ubongo

  • Madaktari wanaweza kugundua mtoto ana kichwa kidogo kabla ya kuzaliwa wakati wanafanya kipimo cha kawaida cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa kijusi

  • Hakuna tiba ya kichwa kidogo, lakini matibabu yanaweza kuwasaidia watoto katika kuongeza uwezo wao

Je, nini husababisha kichwa kidogo?

Sababu za kichwa kidogo ni pamoja na:

Je, dalili za kichwa kidogo ni zipi?

Mtoto anakuwa na kichwa kidogo kinachoonekana. Dalili zingine za kichwa kidogo hutegemea na kiwango cha uharibifu au udumavu wa ubongo. Dalili zinajumuisha:

  • Vifafa

  • Kuchelewa kwa ustawi

  • Matatizo ya kula

  • Matatizo ya kusikia au kuona

  • Matatizo ya kutembea au usawa

  • Kukosa utulivu 

  • Ulemavu wa akili

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto ana kichwa kidogo?

Madaktari wanaweza kufahamu ikiwa mtoto ana kichwa kidogo pale wanapofanya kipimo cha kawaida cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kati ya awamu ya mwisho ya kipindi cha 2 cha miezi mitatu na mwanzoni mwa kipindi cha 3 cha miezi mitatu za ujauzito. Ikiwa madaktari watahisi uwepo wa hali ya kichwa kidogo mara baada ya mtoto kuzaliwa, madaktari watafanya:

  • MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) au uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) wa ubongo

  • Vipimo vya damu

Je, madaktari hutibu vipi hali ya kichwa kidogo?

Hakuna tiba ya kuponya au matibabu ya kawaida ya kichwa kidogo. Matibabu yanaweza kujumuisha:

  • Kutibu dalili zitokanazo na uharibifu wa ubongo

  • Uchukuaji wa hatua za mapema, ambapo huwapatia matibabu watoto ili kuboresha uwezo wao wa kimwili na kiakili