Maambukizi ya virusi vya Zika ni nini?
Maambukizi ya virusi vya Zika karibu kamwe kuwafanya watoto au watu wazima wagonjwa sana. Lakini virusi vya Zika ni hatari sana kwa mtoto ambaye hajazaliwa (kijusi).
Zina inaweza kuenezwa na mbu, ngono au kuongezewa damu
Mwanamke mjamzito aliye na maambukizi ya Zika anaweza kuipitisha kwa mtoto wake
Watu wengi hawana dalili au wanapata tu dalili kidogo, kama vile homa, upele, maumivu ya viungo na macho nyekundu
Watoto waliozaliwa na mama walioambukizwa na virusi vya Zika wanaweza kuwa na kasoro za kuzaliwa kwenye ubongo wao, ikijumuisha kichwa kidogo visivyo kawaida (maikrosefali)
Hakuna matibabu ya maambukizi ya virusi vya Zika, lakini mapumziko na asetaminofeni ili kutuliza homa na maumivu inaweza kusaidia
Je, watu hupata maambukizi ya virusi vya Zika vipi?
Virusi vya Zika vinaenezwa kwa sana na:
Mbu
Virusi vya Zika pia zinaweza kuenezwa kwa:
Ngono
Kuongezewa damu
Mwanamke mjamzito kwa mtoto wake kabla ya kuzaliwa
Ikiwa umeambukizwa virusi vya Zika, unaweza kuieneza kwa mpenzi wako wakati wa ngono:
Hata kama hauna dalili
Kabla dalili zianzie
Wakati unapata dalili
Wiki au hata miezi baada ya dalili zako kuisha—virusi vya Zika vinaweza kukaa kwenye shahawa ya mwanaume kwa hadi miezi 6
Mbu ambazo hueneza virusi vya Zika wanaishi katika tabia ya nchi yenye joto. Kwa hivyo maambukizi mengi ya Zika katika Amerika Kusini na Caribbean. Hata hivyo, watu ambao wanatembelea maeneo hayo kutoka kwa sehemu zingine za ulimwengu wanaweza kurudi nyumbani wakiwa na maambukizi ya Zika.
Je, dalili za maambukizi ya virusi vya Zika ni zipi?
Unaweza kutokuwa na dalili zozote au dalili kidogo. Kwa kawaida dalili hukaa siku 4 hadi 7 na zinajumuisha:
Homa
Upele mwekundu ulioinuka
Maumivu kwenye viungo na misuli yako
Macho mekundu, yanayowasha
Maumivu ya kichwa
Je, Zika huathiri watoto vipi?
Image courtesy of Centers for Disease Control and Prevention, National Center on Birth Defects and Developmental Disabilities.
Mambukizi ya virusi vya Zika wakati wa ujauzito yanaweza kusababisha kasoro za kuzaliwa za ubongo wa mtoto, ikjumuisha kichwa kidogo kisicho cha kawaida (maikrosefali). Watoto walio na maikrosefali wanaweza kuwa na matatizo kama vile:
Vifafa
Kuchelewa katika ukuaji (kwa mfano, wanaweza kuketi, kusimama na kutembea baadaye kuliko kawaida)
Uwezo wa akili uliopungua
Matatizo ya mwendo na usawa
Matatizo ya kula au kumeza
Matatizo ya kusikiliza au kuona
Madaktari wanaweza kujua aje ikiwa nina maambukizi ya virusi vya Zika?
Madaktari wanatambua Zika kulingana na:
Vipimo vya damu
Vipimo vya mkojo
Madaktari wanatibu aje maambukizi ya virusi vya Zika?
Sasa hivi, hakuna dawa ya tiba ya maambukizi ya virusi vya Zika.
Daktari atakuelekeza:
Kupumzika
Kunywa viowevu ili kuhakikisha kuwa kuna maji ya kutosha kwenye mwili wako
Kutumia asetaminofeni ili kutuliza maumivu na homa
Usikunywe aspirini au ibuprofen isipokuwa kama umeonea daktari na unajua kwa hakika kuwa una maambukizi ya virusi vya Zika. Ikiwa una homa ya dengue, ambayo inaweza kuwa na dalili zinazofanana na za Zika, kunywa aspirini au ibuprofen inaweza kuwa hatari na kusababisha kuvuja damu.
Ikiwa wewe ni mjamzito, madaktari wanaweza:
Kufanya atrasonografia kila wiki 3 au 4 ili kuangalia mwendeleao wa mtoto wako
Je, ninawezaje kuzuia maambukizi ya virusi vya Zika?
Njia zile bora zaidi za kuzuia maambukizi ya virusi vya Zika ni:
Kuepuka kung'atwa na mbu
Kuepuka kushiriki ngono na mpenzi ambaye ana maambukizi
Ili kuepuka kuumwa na mbu:
Valia suruali na mashati yenye mikono mirefu
Kukaa kwenye maeneo ambayo yana kiyoyozi au madirisha na vioo vya mlango ili kufungia mbu nje au kutumia neti ya kitanda ya kuzuia mbu
Kutumia vifukuza wadudu ambacho kina DEET (diethyltoluamide) kwenye ngozi isiyofunikwa—lakini usitumie vifukuza wadudu kwa watoto walio chini ya umri wa miezi 2
Tibu mavazi na vifaa vya kuvaliwa kwa kiua wadudu cha permethrin (usiiweke moja kwa moja kwenye ngozi yako)
Wanawake wajawazito wanapaswa kuepuka kusafiri katika maeneo ambayo virusi vya Zika vinapatikana kwa wingi (Tazama Maelezo ya Kusafiri ya Zikaya hivi karibuni).
Ikiwa wewe ni mjamzito na mpenzi wako wa ngono anaishi katika au husafiri kwenye eneo ambalo maambukizi ya virusi vya Zika ni ya kawaida, unapaswa kufanya mojawapo ya yafuatayo wakati wa ujauzito:
Usishiriki ngono (kwenye uke, tundu la haja kubwa au mdomo)
Tumia kizuia mimba chenye vigezo kila mara (kama vile kondomu au kifaa kinachowekwa mdomoni) wakati wa kushiriki ngono
Ikiwa mpenzi wako wa ngono wa kike ametambuliwa kuwa na Zika au ana dalili za Zika, unapaswa kufanya mojawapo ya yafuatayo:
Kukosa kushiriki ngono kwa angalau wiki 8
Kutumia kondomu au vifaa vya kuwekwa mdomoni wakati wa ngono
Ikiwa mpenzi wako wa ngono wa kiume ametambuliwa kuwa na Zika au ana dalili za Zika, unapaswa kufanya mojawapo ya yafuatayo:
Kukosa kushiriki ngono kwa angalau miezi 6
Tumia kondomu unaposhiriki ngono
Virusi vya Zika hukaa kwenye shahawa ya mwanaume kwa muda mrefu kuliko kwenye viowevu vingine vya mwili.