Homa ya Dengue

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Dengue ni nini?

Dengue ni maambukizi ya virusi yanayoenezwa na mbu. Aina kali zaidi ya ugonjwa, unaoitwa homa ya damu, husababisha kuvuja damu na inaweza kuwa hatari.

  • Dengue ni ya kawaida zaidi kwenye tropiki na tropiki ndogo kama vile Upande wa Kusini wa Asia, Amerika Kusini na ya Kati na Caribbean

  • Unaweza kupata dengue uking'atwa na mbu aliye na maambukizi

  • Dalili zinajumuisha homa, kuumwa na kichwa na maumivu ya mwili

  • Unaweza kupata dengue zaidi ya mara moja

  • Ikiwa unasafiri kwenye eneo lililo na dengue, unapaswa kuchukua hatua za kuzuia kung'atwa na mbu

Ni nini husababisha dengue?

Dengue inasababishwa na virusi vya dengue. Virusi hivi vipo katika sehemu za tropiki na subtropiki za ulimwengu kwa sana. Ni ya kawaida zaidi katika upande wa Asia Kusini na Karibi. Lakini watu wachache wamepata dengue katika Marekani kusini na Hawaii.

Wakati mbu anamng'ata mtu aliyeambukizwa, huchukua virusi na kuambukiza mtu mwingine atakayeng'ata.

Je, dalili za dengue ni zipi?

Kwa siku 2 hadi 3, utahisi mdhaifu na mchovu na uwe na:

  • Homa kali na mzizimo

  • Maumivu makali ya kichwa

  • Maumivu unaposogeza macho yako

  • Maumivu makali kwenye mgongo, miguu na viungo vyako—hivi ni chungu sana hadi dengue ukapewa “homa ya kuvunja mifup” kama jina la utani

  • Upele kwenye uso wako

Baada ya kuwa na dalili hizi, unaweza kuhisi vizuri kwa siku na kisha homa na upele unaweza kurejea, wakati huu kwenye kifua, mgongo, mikono na uso wako.

Katika matukio kali zaidi, watu wanaweza kuhisi udhaifu kwa wiki kadhaa, lakini ni nadra kufariki kutokana na homa ya dengue.

Homa ya damu ni nini?

Homa ya damu ya dengue ni aina kali zaidi ya dengue. Huathiri zaidi watoto walio na umri wa chini ya miaka 10 katika maeneo ambayo kidingapopo ni ya kawaida.

Ikiwa una homa ya damu ya dengue, una dalili za dengue na pia:

  • Kuvuja damu kutoka kwenye pua, mdomo, rektamu yako na majeraha ya kutobolewa

  • Maumivu tumboni mwako

  • Kutapika damu

  • Damu kwenye kinyesi au kwenye mkojo wako

  • Alama zenye rangi ya zambarau kwenye ngozi yako kutokana na kuvuja damu chini ya ngozi yako

  • Shinikizo la chini zaidi la damu (mshtuko)

Nenda kwenye hospitali mara moja ikiwa una dalili za homa ya damu ya dengue.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina dengue?

Madaktari wanashuku dengue kulingana na dalili zako na ikiwa umekuwa kwenye eneo ambalo mbu hubeba maambukizi. Kwa kuthibitisha, daktari atafanya vipimo vya damu.

Madaktari hutibu dengue vipi?

Hakuna dawa ya kuua virusi vya dengue. Madaktari watafanya:

  • Watakwambia utumie dawa, kama vile asetaminofini ili kutuliza maumivu na kupunguza homa yako

  • Watakupa viowevu vya IV (kwenye mshipa wako), haswa ikiwa una homa ya damu ya dengue.

Usitumie aspirini au ibuprofeni kwa sababu zinaweza kusababisha kuvuja damu au kuifanya mbaya zaidi.

Madaktari watakuweza chini ya neti za mbu wakati uko mgonjwa ili mbu zisichukue maambukizi kutoka kwako na kuyaeneza kwa watu wengine.

Je, ninawezaje kuzuia dengue?

Ikiwa unaishi au kutembea eneo lililo na dengue, chukua hatua ili kuzuia kung'atwa na mbu:

  • Nyunyiza ngozi yako na dawa ya wadudu ya DEET (diethyltoluamide).

  • Tumia vyandarua

  • Valia suruali na mashati yenye mikono mirefu

  • Kuweka vioo kwa madirisha na kurekebisha mashimo yoyote

  • Kuondoa maji yoyote yasiyosonga katika na karibu na nyumbani ambapo mbu huzaana

Nchini Marekani, chanjo ya kidingapopo imepitishwa kwa matumizi ya watoto ambao

  • Wana umri wa miaka 9 hadi 16

  • Wamekuwa na dengue hapo awali, na

  • Wanaishi katika eneo ambalo dengue imeenea (hutokea mara kwa mara au kwa kuendelea)

Nchini Marekani, maeneo yenye ugonjwa huo ni pamoja na baadhi ya maeneo na majimbo yanayohusiana kwa hiari, kama vile Puerto Rico. Chanjo haijaidhinishwa kwa wasafiri ambao wanatembea lakini hawaishi katika eneo ambalo dengue ni ya kawaida. Chanjo inapatikana pia katika Meksiko, Brazili, Tailandi na baadhi ya nchi zingine.

Chanjo nyingine ya kidingapopo inatathminiwa nchini Marekani na tayari imeidhinishwa kutumika Indonesia, Umoja wa Ulaya na Uingereza. Chanjo hii inaweza kutumika kwa watu ambao hawajapata maambukizi ya kidingapopo hapo awali pamoja na wale ambao wameambukizwa. Chanjo nyingine nyingi za kidingapopo zinachunguzwa.