Uzuiaji Mimba kwa Kuzuia Mbegu za Kiume

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2023

Kingamimba ni kitu kinachotumiwa kuzuia ujauzito (mbinu ya kupanga uzazi). Unaweza kupata ujauzito licha ya kutumia njia za kupanga uzazi, lakini kutumia njia hizo ifaavyo hupunguza uwezekano wa kushika mimba.

Ni nini maana ya kingamimba ya kuzuia mbegu za kiume?

Kingamimba ya kuzuia mbegu za kiume ni aina ya kupanga uzazi inayofanya kazi kwa kuzuia mbegu za kiume zisifikie yai la kike.

Kingamimba za kuzuia mbegu za kiume zinajumuisha:

  • Kondomu

  • Viwambo

  • Vijichupa vya shingo ya kizazi

  • Sponji za kuzuia ujauzito

  • Dawa ya kudhibiti mbegu za kiume

Kuzuia Ufikiaji: Uzuiaji Mimba kwa Kuzuia Mbegu za Kiume

Kingamimba za kuzuia mbegu za kiume huzuia mbegu za kiume zisiingie kwenye uterasi ya mwanamke. Zinajumuisa kondomu, kiwambo, kizibo cha mlango wa kizazi na sponji ya kikingamimba. Baadhi ya kondomu huwa na dawa za kudhibiti mbegu za kiume. Dawa za kudhibiti mbegu za kiume zinapaswa kutumiwa pamoja na kondomu na mbinu zingine za kingamimba ambazo hazina dawa hizo tayari.

  • Mbinu ya kingamimba ya kuzuia mbegu za kiume inayofanya kazi vizuri zaidi ni kondomu ya kiume ya mpira (unapoitumia kwa njia sahihi)

  • Kondomu za mpira ndizo mbinu ya pekee ya kupanga uzazi ambayo pia inalinda dhidi ya magonjwa ya kawaida ya STI (maambukizi ya zinaa), ikiwa ni pamoja na Virusi vya Ukimwi

  • Unaweza kununua kondomu, sponji za kingamimba, na dawa ya kudhibiti mbegu za kiume dukani (bila agizo la daktrai)

  • Viwambo na vizibo vya mlango wa kizazi ni vya ukubwa tofauti na vinapaswa kupendekezwa na daktari

  • Unapaswa kutumia dawa ya kudhibiti mbegu za kiume (kemikali inayoua mbegu za kiume) pamoja na mbinu zote za kupanga uzazi za kuzuia mbegu za kiume

Ninawezaje kutumia mbinu za kupanga uzazi kwa kuzuia mbegu za kiume?

Kondomu

Kondomu ni mipira myembamba inayowekwa kwenye uume (kondomu za kiume) au kwenye uke (kondomu za kike). Aina zote mbili huzuia mbegu za kiume zisiingie kwenye uke. Kondomu zinaweza kutengenezwa kwa mpira, polyurethane, au ngozi ya mwanakondoo. Kondomu za mpira ndizo aina ya pekee ambayo pia inakulinda dhidi ya Magonjwa ya Zinaa ya kawaida.

Kondomu ni lazima zitumiwe kwa usahihi ili zifanye kazi. Kondomu zinapaswa kuvaliwa kabla ya kupenya.

Ili kutumia kondomu ya kiume:

  • Tumia kondomu mpya kwa kila tendo la ngono

  • Tumia kondomu ya ukubwa sahihi

  • Kuwa makini na kondomu ili kuepuka kuiharibu kwa kucha, meno au vitu vingine vyenye ncha kali

  • Vaa kondomu baada ya uume kusimama na kabla ya kugusana sehemu za siri na mwenzi

  • Angalia uone ni upande gani kondomu imekunjwa kwa kuiweka kwenye kidole cha shahada na kujaribu kuikunjua taratibu, lakini kidogo tu

  • Ikiwa haikunjuki, igeuze, jaribu upande mwingine, kisha uikunje tena

  • Weka kondomu iliyokunywa juu ya ncha ya uume uliosimama

  • Acha inchi 1/2 kwenye ncha ya kondomu ili kukusanya shahawa

  • Kwa mkono mmoja, bana hewa iliyonaswa itoke kwenye ncha ya kondomu

  • Ikiwa hujatahiriwa, rudisha nyuma ngozi ya mbele kabla ya kukunjua kondomu

  • Tumia mkono mwingine kukunjua kondomu kwenye uume hadi chini kabisa kisha ulainishe mapovu yoyote ya hewa

  • Hakikisha kwamba mafuta ya kulainisha yapo ya kutosha wakati wa ngono

  • Kwenye kondomu za mpira, tumia tu vilainishi vinavyotokana na maji (vilainishi vinavyotokana na mafuta, kama vile mafuta ya grisi, mafuta ya uokaji, mafuta ya madini, mafuta ya kuchua misuli, losheni ya mwili na mafuta ya kupikia vinaweza kudhoofisha mpira na kusababisha kondomu kupasuka)

  • Shikilia kondomu vizuri kwenye sehemu ya chini ya uume wakati wa kuutoa ili kuzuia kumwaga shahawa

Ili kutumia kondomu ya kike:

  • Weka kishikizo cha upande wa ndani cha kondomu ya kike ndani ya uke kwa umbali unaowezekana bila kuingiza kishikizo cha upande wa nje

  • Sukuma uume kwenye pochi kwa umakini kupitia kishikizo cha nje

  • Iwapo uume utateleza utoke kwenye pochi au kishikizo cha nje kisukumwe ndani, ondoa kondomu ya kike kisha uiweke tena mradi mwanamume asiwe amemwaga

  • Baada ya kumwaga, toa uume nje

  • Bana kishikizo cha nje pamoja na ukipinde ili shahawa isimwagike

  • Kwa umakini, toa kondomu ya kike iliyotumika kwenye uke

  • Itupe

Tumia kondomu mpya kila mara unaposhiriki tendo la ngono, na kamwe usitumie kondomu iliyozeeka au ambayo huenda ina shimo. Dawa ya kudhibiti mbegu za kiume hufanya kondomu zifanye kazi vizuri zaidi, kwa hivyo iweke kila mara unapotumia kondomu mpya.

Viwambo

Kiwambo ni kijikombe cha mpira chenye umbo la kuba kinachosukumwa ndani ya uke hadi kwenye mlango wa kizazi ili kuzuia mbegu za kiume. Shingo ya kizazi ni sehemu ya chini ya uterasi yako. Utapata dayaframu kutoka kwa daktari wako, atakayehakikisha kuwa umepata ukubwa unaokufaa na akufundishe jinsi ya kuitumia. Wewe na mwenzi wako hampaswi kuhisi dayaframu hiyo ikishawekwa.

Dayaframu hukusaidia kuzuia ujauzito, lakini haziwezi kukulinda dhidi ya Magonjwa ya Zinaa.

Ili kutumia dayaframu:

  • Paka krimu au mafuta ya kuua mbegu za kiume upande wa ndani wa kijichupa

  • Ingiza dayaframu kabla ya kushiriki tendo la ngono

  • Usitoe dayaframu kabla ya saa 6 hadi 8 baada ya tendo la ngono (lakini usikae nayo kwa zaidi ya saa 24)

  • Ukishiriki tena tendo la ngono dayaframu ikiwa ndani, ongeza dawa ya kudhibiti mbegu za kiume kwenye uke kwanza

Unaweza kuosha na kutumia tena dayaframu yako. Unapaswa kuangalia dayaframu mara kwa mara ili uone iwapo imechanika. Huenda ukahitaji dayaframu ya ukubwa tofauti iwapo:

  • Umeongeza au kupoteza zaidi ya aunsi 10

  • Umetutumia dayaframu kwa zaidi ya mwaka mmoja

  • Umejifungua mtoto au kutoa mimba

Vijichupa vya shingo ya kizazi

Kizibo cha mlango wa kizazi ni kijikombe cha silikoni chenye umbo la kofia ambacho kinafanana na kiwambo lakini ni kidogo. Kijikombe hicho husukumwa ndani ya uke hadi kwenye mlango wa kizazi ili kuzuia mbegu za kiume.

Unaweza kupata kizibo cha mlango wa kizazi kutoka kwa daktari wako, atakayehakikisha kuwa umepata ukubwa unaokufaa.

Ili kutumia kizibio cha mlango wa kizazi:

  • Paka krimu au mafuta ya kuua mbegu za kiume upande wa ndani wa kijichupa

  • Ingiza kizibio cha mlango wa kizazi kabla ya kushiriki tendo la ngono

  • Usitoe kizibio cha mlango wa kizazi kwa angalau saa 6 baada ya tendo la ngono, lakini usikae nacho kwa zaidi ya saa 48

Unaweza kuosha na kutumia tena kizibo chako cha mlango wa kizazi kwa mwaka 1.

Sponji za kuzuia ujauzito

Sponji ya kingamimba ni sponji yenye dawa ya kudhibiti mbegu za kiume inayowekwa ndani ya uke ili kuzuia mbegu za kiume zisiingie kwenye uterasi. Sponji za kingamimba hukusaidia kuzuia ujauzito, lakini haziwezi kukulinda dhidi ya Magonjwa ya Zinaa.

Unaweza kupata sponji ya kingamimba dukani bila kumwona daktari. Wewe na mwenzi wako hampaswi kuhisi sponji hiyo ikishawekwa.

Unaweza kuingiza sponji ya kingamimba kwa hadi saa 24 kabla ya kushiriki tendo la ngono.

Ili kutumia sponji ya kingamimba:

  • Lowanisha sponji na maji

  • Ikunje na uisukume ndani kabisa kwenye uke

  • Shiriki kitendo cha ngono mara nyingi utakavyo sponji ikiwa ndani

  • Usitoe sponji kwa angalau saa 6 baada ya tendo la ngono, (lakini usikae nayo kwa zaidi ya saa 30)

Matatizo yanayoweza kutokea wakati wa kutumia sponji za kingamimba:

  • Mmenyuko wa mizio

  • Kukauka au maumivu kwenye sehemu ya uke

  • Ugumu wa kutoa sponji

Dawa za kudhibiti mbegu za kiume

Dawa za kudhibiti mbegu za kiume ni kemikali zinazoua manii. Dawa za kudhibiti mbegu za kiume zinapatikana katika muundo wa povu, jeli, krimu au vidonge (dawa laini yenye umbo la tembe inayoweza kuyeyuka ambayo huwekwa kwenye uke). Unapaswa kuweka dawa ya kudhibiti mbegu za kiume kwenye uke wako kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Kwa sababu kidonge ni lazima kiyeyuke, unapaswa kukiweka angalau dakika 10 hadi 30 kabla ya kushiriki tendo la ngono.

Usitumie dawa za kudhibiti mbegu za kiume zaidi ya mara moja kwa siku. Zinaweza kudhuru sehemu ya uke, hali inayoongeza hatari ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi.

  • Hupaswi kutumia dawa za kudhibiti mbegu za kiume pekee yake kama mbinu ya kupanga uzazi—zitumie pamoja na mbinu ya kuzuia mbegu za kiume, kama vile kondomu au dayaframu

  • Ijapokuwa dawa za kudhibiti mbegu za kiume huua manii, haziui vidudu vinavyosababisha Magonjwa ya Zinaa