Limfanjaiktasia ya utumbo ni nini?
Mfumo wa limfu ni mtandao wa mishipa kwenye mwili wako wote. Mishipa hii hutoa majimaji ya ziada, seli mfu na viini vya maradhi. Mishipa ya limfu kwenye utumbo wako mdogo inasaidia kufyonza mafuta na protini kutoka kwenye mlo wako.
Limfanjaiktasia ya utumbo ni hali ya mishipa ya limfu kutokuwa ya kawaida, mikubwa kwenye utumbo mdogo. Mishipa ya limfu inapanuka kwa sababu imezibwa. Kuziba kwa mishipa ya limfu kunasitisha utumbo wako mdogo usifyonze vizuri mafuta na protini. Kutofyonza virutubishi kunajulikana kama hali ya kushindwa kunyonya virutubishi.
Unaweza kuzaliwa ukiwa na limfanjaiktasia ya utumbo, au inaweza ikaanza katika utu uzima kutokana na changamoto ya matatizo mengine
Dalili zinajumuisha kinyesi cha kuhara ambacho kina mafuta na kinanuka na kuvimba kwa miguu yako
Watoto waliozaliwa na limfanjaiktasia ya utumbo hawatakua kama kawaida na watakuwa wafupi na wenye uzani wa chini
Madaktari wanatibu kisababishi cha tatizo ikiwa inawezekana
Ili kusaidia kutibu dalili zako, unaweza kula kiwango kidogo cha mafuta na ule zaidi protini na kutumia vidonge vya virutubishi
Nini kinachosababisha limfanjaiktasia ya utumbo?
Kisababishi kikubwa kwa watoto wachanga na watoto ni:
Kuzaliwa na mishipa ya limfu ikiwa haijajiumba vizuri
Watu wazima wanaweza kupata limfanjaiktasia ya utumbo ikiwa wana:
Saratani au matatizo mengine ambayo yanaweza kuziba mishipa ya limfu kwenye tumbo
Dalili za limfanjaiktasia ya utumbo ni zipi?
Dalili zinajumuisha:
Kuvimba kwenye mguu mmoja au yote miwili
Kuharisha
Kuhisi mgonjwa tumboni na kutapika
Kinyesi chenye mafuta
Maumivu ya tumbo
Kukua taratibu kwa watoto
Madaktari wanawezaje kujua iwapo nina limfanjaiktasia ya utumbo?
Madaktari hufanya vipimo, ikiwemo:
Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi kutoka kwenye utumbo mdogo
Wakati mwingine limfangiografia ya kulinganisha
Kwa kufanya kuondoa kipande kidogo cha utumbo mdogo kwa ajli ya uchunguzi, madaktari wanachukua sampuli ndogo ya tishu kwa kutumia vifaa mwishoni mwa endoskopi (bomba rahisi la kutazamia). Kisha wanaiangalia sampuli hiyo kwa kutumia hadubini.
Kwa ugonjwa wa limfangiografia ya kulinganisha, madaktari wanafanya vipimo vya eksirei vya mishipa yako yote ya limfu baada ya kudunga dutu ya kuboresha picha kwenye mishipa ya limfu kwenye mguu wako. Majimaji yenye kutofautisha hufanya mishipa yako yote ya limfu ionekane kwenye eksirei.
Madaktari pia watafanya vipimo vya damu ili kuangalia ikiwa kuna matatizo.
Je, madaktari wanatibu vipi limfanjaiktasia ya utumbo?
Madaktari hutibu kisababishaji cha limfanjaiktasia ya utumbo ikiwa inawezekana
Dalili zako zinaweza kupata unafuu kwa:
Kula lishe yenye mafuta kidogo na protini nyingi
Kutumia vidonge vya virutubishi vya kalsiamu na vitamini
Kutumia aina fulani za fati zinazoitwa mnyororo wa kawaida wa trigliseridi (MCTs) ambazo ni ndogo kuweza kunyonywa moja kwa moja kwenye utumbo mdogo na haipiti kwenye mfumo wa limfu
Wakati mwingine, upasuaji kwenye utumbo mdogo au mshipa wa limfu uliozuiwa inaweza kusaidia.