Matumbo yako ni utumbo wako. Una utumbo mpana na utumbo mdogo. Chakula hufyonzwa kwenye sehemu ya utumbo wako mdogo.
Hali ya kushindwa kunyonya virutubishi ni pale mwili unashindwa kumeng'enya virutubishi katika chakula chako. Virutubishi ni vitu vinavyotosheleza mwili wako. Vinajumuisha protini, wanga, mafuta, vitamini, na madini.
Ugonjwa wa utumbo mfupi ni nini?
Ugonjwa wa utumbo mfupi ni tatizo ambalo unalipata ikiwa ulifanyiwa upasuaji ambao uliondao sehemu kubwa ya utumbo wako mdogo.
Ikiwa huna utumbo mdogo wa kutosha, huwezi kunyonya virutubishi vya kutosha
Utapungua uzani na kupata utapiamlo
Pia utapata gesi na kuhara
Kurekebisha mlo wako na kutumia dawa fulani kunaweza kusaidia kupunguza kuhara
Baadhi ya watu wenye utumbo mdogo mfupi sana wanahitaji kulishwa kupitia mishipa
Nini kinachosababisha ugonjwa wa utumbo mfupi?
Ugonjwa wa utumbo mfupi unatokea baada ya sehemu kubwa ya utumbo mdogo kuondolewa wakati wa upasuaji. Sababu za kawaida za kuondoa sehemu ya utumbo wako mdogo ni:
Mesenteriki iskemia (ateri iliyofungwa inayopeleka damu kwenye sehemu kubwa ya utumbo mdogo)
Jeraha kwenye utumbo kutokana na tiba ya mionzi
Volvulasi (sehemu iliyojifunga ya utumbo)
Kasoro za kuzaliwa
Dalili za ugonjwa wa utumbo mfupi ni zipi?
Dalili zinajumuisha:
Kuharisha
Kupungua uzani
Kushindwa kunyonya vitamini na madini ya kutosha
Upungufu wa vitamini na madini unaweza kusababisha:
kiwango cha chini cha damu (anemia)
Kuchubuka kwa urahisi
Kuwashwa mikono na miguu
Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nina ugonjwa wa utumbo mfupi?
Madaktari wanatambua kuwa una ugonjwa wa utumbo mfupi kulingana na dalili zako pamoja na ukweli kwamba sehemu kubwa ya utumbo wako mdogo iliondolewa.
Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa utumbo mfupi?
Ikiwa una ugonjwa wa utumbo mfupi, huenda ukahitaji:
Dawa za kupunguza kuharisha
Mlo kiasi kidogo, mara kwa mara ukiwa na protini zaidi na fati na kabohaidreti kidogo
Virutubisho vya lishe, ikiwa ni pamoja na vitamini, kalsiamu na magnesiamu
Dawa za kuzuia asidi kwa ajili ya tumbo lako ikiwa litaanza kuzalisha asidi nyingi sana
Ikiwa matibabu haya hayatakufanya uvumilie kula, madaktari huenda:
Wakakulisha kupitia mishipa kwa kudumu (hutwa TPN [lishe kupitia mishipa kikamilifu])
Wakati mwingine, madaktari wanaweza kukubadilishia utumbo mdogo kutoka kwa mtu ambaye amekufa.